Jeshi la S.Kusini lakomboa Malakal


Mazungumzo ya amani kati ya serikali na waasi yamekwama mjini Addis Ababa
Jeshi la Sudan Kusini linasema kuwa limeukomboa mji muhimu wa Malakal kutoka kwa waasi.
Msemaji wa jeshi Phillip Aguer amesema kuwa vikosi vya serikali vimewatimua waasi kutoka mji huo ambao ndio mji mkuu wa jimbo la Unity lenye utajiri mkubwa wa mafuta.
Wakati huohuo mji wa Bor ulikombolewa hivi karibuni na wanajeshi wa Serikari umedaiwa kuharibika kufuatia mapambano na waasi.
Lakini msemaji wa waasi, Brigedia-Generali Lul Ruai, amekanusha ripoti hizo ikisema kuwa waasi wangali wamuteka mji huo.
Ukombozi huu unakuja siku mbili baada ya wanajeshi kukomboa mji wa Bor.
Waandishi wa habari wanasema kwamba ikiwa ni kweli serikali imekomboa Malakal, mji wa mwisho mkubwa uliokuwa umesalia chini ya waasi, huenda hatua hiyo ikakwamua mazungumzo ya amani ya pande zote mjini Addisa Ababa, Ethiopia.
Waasi hata hivyo wangali wanadhibiti baadhi ya sehemu za nchi hiyo hasa maeneo ya vijijini.
Na BBCSwahili