Watu 28 wauwawa Iraq

Msururu wa miripuko ya mabomu nchini Iraq umesababisha vifo vya watu 28 hii leo.
Afisa mmoja wa serikali amedai kwamba wapiganaji wanaofungamana na wapiganaji wa Alqaeda wamejikita katika mji waliouteka mwezi uliopita na kuingiza silaha nzitonzito za kutosha kuvamia mji mkuu wa taifa hilo.
Miripuko hiyo ya mabomu iliyosikika zaidi katika mji wa Baghadad imelenga maeneo ya masoko na majengo ya mahakama imeshuhudiwa katika wakati ambapo jeshi limekuwa likifanya operesheni ya kujaribu kuliteka tena eneo hilo hapo jana.
Jeshi hilo hata hivyo limekabiliwa na upinzani mkali wa wanamgambo.
Tangu mwezi wa Desemba wanachama wa tawi la Al Qaida nchini Iraq linalojulikana kama dola la kiislamu la Irac limeidhibiti sehemu ya mji wa Ramadi ambao ni mji mkuu wa jimbo linalokaliwa na idadi kubwa ya wasunni la Anbar magharibi ya Iraq.
Na Dw.deSwahili