RAIS Hassan Rouhani wa Iran amesema
leo hii haki za nchi hiyo za kurutubisha madini ya urani ni mistari mekundu
ambayo haiwezi kuvukwa na kwamba Jamhuri hiyo ya Kiislamu ilitumia busara
wakati wa mazungumzo kuhusu mpango wa nuklea wa nchi hiyo.
Rais wa Iran Hassan Rowhani |
Akizungumza katika bunge la taifa
amesema wamewaeleza wajumbe wanaozungumza nao kuhusu mpango huo wa nuklea
kwamba hawatosalimu amri kwa vitisho vyovyote vile,vikwazo, hila au kwa
kubaguliwa na kwamba nchi hiyo haikuinamisha na haitoinamisha kichwa chake
kutokana na vitisho kutoka mamlaka yoyote ile.
Amesema kwamba kuna mistari mekundu
ambayo haiwezi kuvukwa na maslahi ya taifa ni mistari mekundu yenye kujumuisha
haki chini ya mifumo ya sheria za kimataifa na kurutubisha urani.
Hapo jana Iran na mataifa sita
yenye nguvu duniani wameshindwa kufikia makubaliano ya kusitisha mpango wa
nuklea wa Iran lakini yamesema tafauti zao zimepunguwa na wataanza tena
mazungumzo katika kipindi cha siku 10 kujaribu kuumaliza mzozo huo uliodumu kwa
muongo mmoja.
By Dw.de