CHAMA cha waalimu
Tanzania CWT kimesema kuwa kinashangwazwa na watu wanao taka kukivuruga na
kuanzisha vyama vinavyo pingana nacho na kufadhiliwa na vigogo wa baadhi ya
vyama vya siasa.
Rais wa CWT, Gration Mukoba |
Akizungunza na waandishi wa hab ari mda mfupi baada ya
kukabidhiwa jingo la chama hicho mkoani Mbeya lililojengwa na Suma-JKT, Rais wa
CWT, Gration Mukoba,
alisema kuwa anashangazwa na kuwapo kwa watu wachache wanao taka kuuvuruga
umoja wao wa chama hicho na kutoa ufadhili kwa wanao meguka kutoka chama hicho.
Alisema kuwa anashangazwa na wanao taka kuuvuruga
umoja huo wa wapiganaji wanao taka kuwapo kwa utengano katika kudai haki za
waalimu ambao wanapigania haki zao kila kukicha ili kuhakikisha wanapata
maslahi yao.
Mukoba alisema kuwa kufuatia uanzishwaji wa vyama
vidogovidogo hapa nchini ambavyo vimekuwa na ushawishi wa kuwatenga waalimu
kutoka katika chama hicho ni kuudhohofisha umoja huo na kunalenga kusababisha
kuwatenga katika upiganaji wa haki zao.
Baadhi ya waalimu wa mkoa wa Mbeya wakimsikiliza Rais wao wakati wa uzinduzi wa jengo lao jijini Mbeya |
Alisema kuwa wanaoanzisha vyama hivyo si bure kuna mtu
kawatuma kufanya hivyo ili kuuvuruga umoja wa waalimu na kuhakikisha hawapati
haki wanazo zipigania kutoka kwa serikali.
“Uanzishwaji wa vyama vingene vya waalimu vinalengo
baja nasi la kuhakikisha tunazoofika katika kupigania haki zetu kutoka
serikalini na kuhakikisha tuna gawanyika vyama hivyo nimesikia vimeanzishwa
Mwanza na hapa Mbeya Nilisikia kuna chama kimeanzishwa” Alisema Mkukoba.
Alisema waalimu wasinge kuwa na ushirikiano na
kujitolea kukatwa pesa kidogo wanazo katwa kutoka katika mishahara yao tusinge
fikia hapa tulipo na kujenga jengo kubwa na kuhakikisha wanazipata hakizao.
Alisema sheria ya Tanzania ina ruhusu kuanzishwa kwa
vyama vya wafanyakazi kama uanaeanzisha chama utakuwa umefikisha wanachama 20
lakini kwa kufanya hivyo kujigawa kutasababisha waalimu kushindwa kudai haki
zetu kwa pamoja.
“Hawa wanao anzisha vyama huko pembeni wametumwa
kutugawa na kutusambaratisha nawasihi waalimu wenzangu msikubari kugawanyika
kutoka katika chama hiki, pia kumekuwa na kampeni za kuwaondoa waalimu wakuu
kutoka katika nafasi mbalimbali za uongozi jambo hili litakuwa ni jema kwani
maamuzi yatakayo tolewa na mwalimu wa kawaida litakuwa la busala kuliko mla
mwalimu mkuu ambaye ataogopa kunyang’anywa ualimu ukuu,’ Aliongeza Mukoba.
Alisema kufuatia hekaheka za kuwaondoa katika uongozi
waalimu wakuu walaka wanao kutoka serikalini ukiwataka waalimu wakuu kutokuwa
na wadhifa wowote katika chama hicho na kiongozi mmoja wa chama hicho kwa mkoa
wa Iringa ameachia ngazi kufuatia walaka huo.
Hivyo chama chao hakiteteleki na uamuzi huo na walaka
wa aina hiyo na kuwa watawaweka vijana ambao sio wakuu wa shule ili kuwa na
watu ambao hawaogopi kufanya halakati za kudai haki.
Alisema kuwa hivi karibuni walikuwa mkutano wao ambao
walijadili mbambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na deni wanaloidai Serikali, na
kuwa wameipa serikali muda wa miezi miwili na kuwa wata washa moto kama kama
wataona iko kimya.
“Tumeipa Serikali muda wa miezi miwili na tukiona kuna
ukimya tutawasha moto tena na kutakuwa na mgomo mkubwa hayo ni baadhi tut a
yale tuliyo fikia muafaka katika mkutano wetu mkuu uliopita,” Alisisitiza
Mukoba.