Anawaambia waandishi wa habari kuwa wamechota maji na kubeba tofari lakini watoto wao hawasomi hapo na kati ya watoto 300 shule nzima watoto chini ya 10 ndio wa kata yao.
Mkazi anaye simulia alivyo tumikia katika ujenzi wa shule hiyo na jinsi watoto wa kata yao ambavyo hawanufaiki na shule hiyo.
Mmoja wa wazazi wenye watoto katika shule ya Anna Makinda akizungumzia jinsi watoto wao wanao soma pale na ada wanayo lipa
Afisa mtendaji wa kijiji cha Ihanga na kaimu afisa mdendaji kata ya ihanga inakopatikana shule ya Anna Makinda akizungumza na waandishi wa habari walio piga kambi kijijini hapo
Mwenyekiti wa kijiji cha Ihanga kata ya Ihanga ilipo shule ya anamakinda
Kibao cha shule
Mazingira ya shule ya Anna Makinda ya wasichana pekee halmashauri ya mji Njombe
Ni kibao cha kuelekea ihanga na vijiji vyake inako patikana shule ya sekondari ya wasichana ya anamakinda
Venance Msungu Afisa elimu sekondali halmashauri ya mji Njombe, asema shule hiyo ni ya halmashauri tofauti na wananchi wanavyo itambua.
WANAWAKE wakazi wa ya
kijiji cha Mkalati kata Ihanga wilaya ya Njombe mkoani hapa wamelalamikia uongozi
wa kata hiyo kuwanyanyasa wakati wa kukusanya michango ya ujenzi wa shule
ambayo wao watoto wao wanaenda kwa asilimia chache huku wakifanya kazi za
ujenzi kama kuchota maji na kufyatua matofari.
Wakizungumza na kituo huki kwa nyakati tofauti kijijini hapo
mkoani Njombe walisema wakekuwa wakifanya ujenzi katika shule ya Anna Makinda
ya wasichana ambayo wameambiwa ni ya kata huku ikichukua wanafunzi kutoka nje
ya kata yao na kudai kuwa kuna watoto hadi kutoka nje ya mkoa wa Njombe
wakizoma katika shule huyo.
Mmoja wa wanawake wa kijiji hicho Theodola Mkombe alisema kuwa
watoto wa kata yao wanao soma katika shule yao ni chini ya watoto 10 kati ya
watoto 300 wa shule hiyo kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne.
Shule hiyo wakati inatambulishwa tuliambiwa kuwa ni shule ya
kata lakini sasa tunashangaa kuona ni shule inayo chukua wanafunzi kutoka
sehemu mbalimbali wakati tulio shiriki ujenzi watoto hawaingii katika shule
hiyo na kusema kuwa wanaona wanaonewa.
“Shule hii ili kuwa inafahamika kama shule ya kata tulijitoa
kwa moyo kuijenga lakini tunashangaa kuna watoto wanatoka mbali wanakuja kusoma
hapa mimi inaniuma watoto wanao soma kutoka shule hii ni wachache, ni watoto
kama sita tu wanao soma katika shule hiyo” alisema Mkombe.
Naye Suzana Malekela alisema kuwa wamekuwa wakibebeshwa maji
wakati wa ujeni na kufyatuo tofari kutoka mtoni na kuzileta shuleni huku
wakiambiwa kuwa shule hiyo ni ya kata yao na walipo kuwa wakianza ujenzi wa
shule hiyo walitaraji watoto wao kunufaika na shule hiyo lakini watoto wao
hawanufaiki na shule hiyo waliyo toa nguvu yao na kuona watoto kutoka sehemu
mbalimbali kuja kuoma hapo.
“Tumebeba maji na kufyatua matofari mpaka sasa hatuna
manufaa na shule hii kwa kuwa watoto wetu ni wachache, pesa zetu tumechanga
lakini watoto wetu hawapati elimu hapo inauma sana,” alisema Malekela.
Aidha kwa mujibu wa wakazi hao walisema kuwa wazazi wote wa
kijiji hicho wanatoa 32,000 kwa mwaka kwa ajili ujenzi wa shule hiyo na kuwa
wanafanya shughuli zingine za ujenzi kama uchimbaji wa mashimo ya vyo katika
shule hiyo.
Hata hiyo afisa mtendaji wa kata ya ihanga na mwenyekiti wa
kijiji hicho Aderhad Mlowe, amesema kuwa kweli wananchi wa kata hiyo wakiwemo
wanawake wamekuwa wakitumia nguvu zao kufanya shuguli za ujenzi na kuwa awali
wakati shule hiyo inaanza kujengwa walitumia nguvu zao na kutoa michango
kwaajili wa ujenzi wakiambiwa kuwa shule hiyo ni ya kata lakini naye anashangaa
kuona watoto wanachulikuwa hata nje ya kata yake.
Alisema kuwa kuwepo kwa mkanganyiko wa shule hiyo kuwa ni ya
kata ama ni ya halmashauri ya Njombe na kusababisha kuwa wakazi wa kijiji hicho
kushindwa kufanya shughuli za kimaendeleo kwa moyo kutokana watoto wao kuwa
wachache katika shule hiyo na kusema kuwa watoto waliopo katika shule hiyo ni
300 lakini watoto wao ni chini ya 10 waliopo shuleni hapo.
Afisa elimu halmashauli ya mji wa Njombe ambeye ndiyo mwenye
shule hiyo Venance Musungu, alipo uliza kuhusu shule hiyo alisema kuwa shule hiyo
ni ya wasichana ya halmashauri na inachukuwa watoto kutoka katika maeneo
mbalimbali ya halmashauli ya mji huo na kuwa shule hiyo wakazi wa kata hiyo wanachangia
kidogo na halmashauri inachangia pesa kwaajili ya ujenzi wa shule hiyo huku
akisema kuwa wakazi hao wanachangia nguvu kazi na halmashauri inachangia pesa
katika ujenzi wake.
Alisema watoto kutoka kata hiyo idadi yao kila msimu
wanachukuliwa zaidi ya sita kwa kila shule ya msingi kutoka kata hiyo lakini
watoto wa kata hiyo wengine wasichana kwa wavurana hupelekwa shule ya kata ya
jirani shule ya Kifanya.
“watoto katika kata ya Ihanga wanawitikio mdogo kielemu hiyo
kutoka kata zingine ndio wanajaa kwa kuwa watoto kutoka kata hiyo hawawezi
kujaza shule hiyo lakini mzazi kama mtoto wake kapelekwa shule ya kata ya
Kifanya aje kuleta maoombi tutamwamishia pale,” alisema Afisa Elimu.
Wakazi wa vijiji vya kata hiyo wanacholalamika ni kuhusiana na
kutoa michango yao wakati shule hiyo watoto wao hawaendi kusoma katika shule
hiyo na kuona wanatoa michango mikubwa ya shilingi 32,000 na kutoa nguvu yao
huku watoto wao wakishindwa kuingua katika shule hiyo.
Aidha mmoka wa wadau wa elimu mkoa wa Njombe na mzaliwa wa
moja ya kijiji katika kata hiyo, Emiliani Msigwa na mtoto wa diwani wa zamani
wa kata hiyo alisema kuwa wakati kata hiyo haija gawanyika kutoka kata ya Kifanya
na baba yake akiwa diwani wa kata hiyo alitoa wazo la kuanzisha shule hiyo
baada ya kuona kuwa wanafunzi wa kike wanashindwa kuendelea na shule katika
shule ya kata ya kifanya kwa kupata mimba hiyo aliona kuanzishwa kwa shule hiyo
ya kata ya wasichana inainua elimu kwa wasichana wa kata hiyo.
“Baba akiwa diwani wa kata ya Kifanya alisema kuwa kutokana
na watoto wakike kuonekana wamefeli na kupata mimba basi aliamua kuanzisha
shule hiyo kwaajili ya kuokoa kizazi cha watoto wakike lakini ninacho shangaa
baadae halmashauli ilipoka shule hiyo lakini zaidi wazazi wanaumizwa kwa
michango mingi, lakini watoto wao ni wachache wanao ingia katika shule hiyo,”
alisema Msigwa.
Hivyo hata wadau wengine wa elimu kata hiyo wameiomba
halmashauli kuilipa kata hiyo kwa kujengewa shule ya kata kwaajili ya wanafunzi
wa wazazi walio changia katika kata ya Ihana huhakikisha wanasoma katika kata
yao ambayo itakuwa ni mbadala wa shule ya Anna Makinda.