MBUNGE la Njombe Magharibi Gerson
Lwenge ametoa onyo kwa wanasiasa ambao wameanza kupiga kampeni wakati yeye bado
hajamaliza mda wake wa ubunge hasa kampeni za usiku na kununuliwa kwa pombe wa
wananchi wake.
Akizungumza kwa nyakati tofauti katika ziara zake za Vijiji
kwa vijiji katika kata za jimboni humo, Lwenge alisema kuwa wananchi wanatakiwa
kuwa makini na watu wa aina hiyo.
“Wananchi muwe makini na watu wanao kuja na kuwapa pombe
katika kampeni zao za usiku kwa kuwa mda wa kampeni bado haujafika na mtafakali
ni kwan ini wanapiga kampeni za usiku,” alisema Lwenge.
Kwanza wananchi mnatakiwa kutafakari ju ya watu wanao kuja
katika maeneo yenu usuku na kuwanunulia pombe na kuanza kuwaambia mmchague
kwani watu hao wanawanunulia pombe lakini pombe hamuwezi kwenda nazo katika
nyumba zenu.
Alisema kuwa mtu akiwafuata na kuwaambia wamchague wamuulize
kuwa amewafanyia nini kwa kuwa wakati wa kuambiwa watafanyiwa mda huo ulipita.
“Wananchi wakati wa kuambiwa mtafanyiwa wakati huo ulipita
miaka ya nyuma, katika kipindi change kuna vijiji vitapatiwa umeme zaidi ya 40
lakini miaka ya hapo nyuma wabunge wawili walipita na vijiji tisa vilipata
umeme, na shule mbili zilipatiwa umeme lakini kwa sasa shule zote za kata
zitapatiwa umeme,” aliongeza Lwenge.
Alisema kuwa katika kipindi chake vijiji vingi vimepata umeme
tofauti na miaka ya utawala wa wabumbe wa kabla yake na kuwa katika utawala huu
vijiji vichache vitachelewa kupata umeme na kupatiwa katika awamu ya tatu.
Alisema kuwa pia katika kipindi hiki amefanikiwa kuwapelekea
barabara wananchi kjwa kiwango cha changalawe na lami kwa baadhi ya maeneo
katika jimbo hilo na kuwa wananchi kwa mda huu wanaweza kuunganishwa kwa
mtandao wa barabara.