TASAF YAWEZESHA WANANCHI WAANZA UFUGAJI


 Mzee Michael Haule Mnufaika na mradi wa Tasaf 3


 Wanufaika wa Tasaf 3
 William Malima mratibu wa Tasaf 3 wilaya ya Ludewa

 baadhi ya mifigo ya wanufaika wa Tasaf 3
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dr Rehema Nchimbi akizungumza na wanufaika wa Tasaf 3 Ludewa

FEDHA zilizotolewa na mfuko wa Tasaf awamu ya tatu kwa ajilia ya kunusuru kaya maskini katika wilaya ya Ludewa zimeanza kuonyesha mafanikio kwa walengwa na kubadilisha maisha yao kwa kuanza kuuaga umaskini ikiwa ni miezi michache baada ya kuzana kutolewa.

Fedha hizo Zlizotolewa kwa kaya maskini 3174 zimeanza kuonyesha mafanikio kwa walengwa na kuanza kuondokana na umaskini kwa kujishughulisha na ufugaji kuku, nguruwe na wengine kuanza ujenzi wa nyumba bora za kuishi.

Wanufaika walishuhudia mabadiliko baada ya kupata fedha na jinsi zilivyo badilisha maisha yao ambapo ambaye hakuwa na kitu kupata kutu na asiye kuwa na mifugo kuanza kufuga

Agnes Nyangoyara alisema kuwa kwa awamu ya kwanza alipata shilingi 20,000, na kujinunulia kuku wawili na kuwa kwa sasa anakuku zaidi ya kumi na kuwa kwa awamu ya pili pesa zake aliziweka na kuongeza zingene na kufikisha shilingi 40,000 ambapo amefyatua tofari na kutengeneza tanuri.

“Fedha za awamu ya pili niliziweka na nika tafuta nyingine na kufikia shilingi 40,000 nemetengeneza tanuli la tofari kwaajili ya kujenga nyumba nikipata pesa nyingine,” alisema Nyangonyara.

Hata hivyo bibi Mona Haule anasema kuwa yeye kwa awamu ya kwanza alipata shilingi 40,000 na kuongeza shilinhi 40,000 na kununua mfugo wa nguruwe ambaye anamfuga nyumbani ambaye anataraji kumuuza kwaajili ya buboresha zaidi maisha yake.

Hata hivyo mzee Michael Haule anasema kuwa pesa hizo zinamsaidia kununua Mbolea kwaajili ya kukuzia mahindi yake na huku akisema kuwa katika shamba lake la Robo heka anatarajia kupata michuko 12 ya mahini wakati wa mavuno.

Mratibu wa Tasaf wilaya ya Ludewa William Malima anasema kuwa wakazi wengi wananufaika na mpango huo na kuwa wameonekana kubadilisha maisha yao kutokana na kufanya juhudi na jinsi walivyo toa elimu ya matumizi ya fedha.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Dr Rehema Nchimbi anawataka maafisa ugani mkoa wa Njombe kuhakikisha kuwa wanawafikia wanufaika na mfuko huo kwaajili ya kuangalia mifugo yao ili isiathiliwe na magonjwa na kuhakikisha kuwa mazao yao yanakuwa na afya kwa kuwapatia elimu ya nini cha kufanya.

“Najua kila wilaya kuna maafisa ugani, maafisa mifungo, nawaagiza watembeleeni wananchi hawa ili wasije pata maafa ya kufiwa na mifugo yao ama madhao yao kuto stawi wakati ninyi mpo kwaajili ya kuwapa ushauri,” alisema Nchimbi