WANANCHI WAOMBA DARAJA LA WILAYA NA WILAYA ILI KUPATA HUDUMA YA AFYA

WANANCHI kwa kijiji cha Kipingu wilayani Ludewa wamemuomba Rais wa jamuhuli ya muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli kwa kuwajengea daraja katika mto Luhuhu linalo unganisha wilaya ya Ludewa mkoani Njombe na na mkoa wa Ruvuma ambako wanapata huduma za afya na mahitaji mengine ya nyumbani.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi hao walisema kuwa wanamuombea Rais kuwasaidia kujenga daraja katika mto Luhuhu linalo unganisha wilaya ya Ludewa mkoani Njombe na wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma ambako kuna hospitali na kupata huduma za afya huko kama alivyo ahidi katika kampeni zake.

Luciana Mapunga alisema kuwa katika wilaya jirani nao ya Mbinga katika kijiji cha Lituhi kuna Hospitali ambako wanaona ni karibu kupata huduma za afya wakati wanapo ihitaji huduma hiyo.

Alisema kuwa kuna zamani walikuw ana kivuko ambacho kilikuwa ni msaada kwao kuvuka na kupata huduma mbalimbali ambacho kilikuwa kina fanya shughuli zake mara kwa mara lakini baada ya kuletewa kivuko kikubwa kimekuwa kikwazo kutokan ana kufanya kazi mara chache na baadhi ya miezi.

“Tunamuomba Rais Magufuli kutujengea daraja katika mto Luhuhu ambao litakalotuunganisha na kijiji cha jilani cha Lituhi Mbinga ambako kuna Hospitali tunako pata huduma ya afya na mahitaji muhimu kama mafuta nyanya na vitu vingine vya matumizi ya kawaida nyumbani, tunamuombea Kwa Mungu ili atujengee daraja hilo,” alisema Philimon Haule.

Alisema kuwa pantone kubwa lililo letwa katika eneo hilo la mto Luhuhu huwa linafanya kazi kwa mwaka ni miezi minne ambayo ni mwezi wa Aprili na mwezi wa julai huku miezi inayo baku kuto fanya kazi.

Hata hivyo wananchi hao walisema kuwa Rais katika kampeni zake aliwaahidi kujengewa daraja katika mto huo badala ya kuwapo kwa kivuko na kumshukuru mungu kwa kuwa amepita.

Joseph Mhagama alisema kuwa katika kijiji hicho wakijingewa daraja watafaninikwa kupata huduma kwa urahisi kutika katika wilaya ya mbimga ambako wanategemea huduma mbalimbali.

Aidha alisema kuwa mbali na kuwapo kwa changamoto hiyo alisema kuwa kuna shida ya maji katika kijiji cha ambapo waliambiwa wachime mitalo ya maji na kuwa ni muda mrefu umepita bila kupata huduma hiyo huku kukiwa na mitalo hiyo.

Alisema kuwa licha ya kuwapo kwa mitaro hiyo pia wananchi hao wanatazama visima visivyo na maji na matanki ambayo hayajaanza kuhufadhi maji baada ya kudaiwa kuwa pampu ya kuvuta maji kutoka katika visima hivyo.