Mkuu wa mkoa; Njombe lindeni historia ya kuto pata kipindupindu kati ya mikoa nane Tanzania

WAKAZI wa mkoa wa Njombe wametakiwa kuendeleza usafi wa mazingira ili kuto iharibu historia yake ya tangu kuanzishwa kwakwe kuto kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu ambapo toka kuanzishwa kwake hakujawahi kutokea mgonjwa wa ugonjwa huo wa aibu.

Wito huoumetolewa na mkuu wa mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi wakati akizindua wiki ya usafi wa mazingira kitaifa mkoani humo, jana na kuwataka wakazi wa mkoa huo kuhakikisha kuwa wanaendelea kuwa wasafi na kuhakikisha kuwa mazingira ya kupatikana kwa ugonjwa huo hayapatikan.

Alisema kuwa amekuwa akisikitika mkoa huo kuonekana tu kinala kwa mamo mabaya lakini ameanza kuingia na faraja kwa kuona unakuwa ni miongoni kwa mikoa nane ambayo ugonjwa wa kipindipindu haujagusa.

Alisema kuwa ugonjwa huo ni wa aibu haipaswi kwa wakazi wa mkoa wa Njombe kupatwa na kuwa waendeleze usafi wa mazingira kwa kuhakikisha kuwa wankuwa na vyoo imara na kuepika kufanya shuguri muhimu bila kunawa.

Alisema kuwa wakazi hao pamoja na kujitahidi kuwa wasafi na halmashauri zake kushika nafasi za juu katika usafi wa mazingira amezitaka halmashauri hizo kuhakikisha kuwa katika ofisi zao kunakuwa na vyoo bora ili kuwa mfano kwa wakazi hao.

Alisema kuwa mkoa huo inatakiwa kuendelea hivyo ili kuwa mfano wa kuigwa na halmashauri zingine za hapa nchini kwa kuja kujifunza mkoani hapo juu ya usafi wa mazingira na uboreshaji wa vyoo.

Aidha alisisitiza kuwa katika kila ofisi kunatakiwa kuwa na choo bora kwa kuwa watu wengine wanaogopa hata kunjwa maji kwa sababu hana pa kuyapeleka akibanwa na haja.

"Mkoa huu umekuwa ukisemwa vibaya katika maambukizi ya Ukimwi lakini kwa sasa napata faraja kwa kuwa kuna kitu kizuri unafanya ni miongono mwa mikoa nane ambayo haijagushwa na Kipindupindu na hakuna anaye penda kupata ugonjwa wa aibu wa kula kinyeshi," Alisema Mkuu wa mkoa Dr. Nchimbi

Hata hivyo aliwaka wahusika wa mamlaka ya maji huhakikisha kuwa maji safi na salama yanapatikana kila wakati kwa wakazi hao kwa kuwa usafi unahitaji kuwepo kwa maji na kusema kuwa wakazi wasiwe na imani ya kuwa waji safi ni ya bomba pekee bali hata ya visima ni maji safi.

Awali akimkaribisha mkuu wa mkoa ofisa afya mkuu kutoka Tamisemi Juma Motoka alisema kuwa wakazi wa Njombe na watanzania kwa ujumla watambue kuwa kupatwa na kipindupindu ujue kuwa umekula kinyesi na si vinginevyo.

Alisema kuwa wakazi hao wahakikishe kuwa wanajikinga na kula vitu ambavyo havija oshwa na maji safi na kuachana na kula vyakula vya baridi kwa kuwa kinyesi kibichi ndicho chenye kipindupindu.

Hata hivyo katibu tawala wa mkoa wa Njombe Jakson Saitabahu alisema katika mkoa huo wamekuwa na kampeni mbalimbali za kufanya usafi katika mkoa huo na kuwa wakazi uzi ulio wakikifa hapo na wasikubali kipindupindi katika mkoa huo.

Wiki ya usafi wa mazingira binafanyika mkoani Njombe kitaifa ambapo ilizinduliwa juzi na mkuu wa mkoa wa Njombe na kifikia kilele chake Novemba 19 mwaka huu