Maadhimisho ya siku ya mazingira duniani kotaifa kufanyika mkoani Njombe

WANANCHI mkoani Njombe wanatarajia kuwa wenyeji wa maadhimisho wiki ya usafi wa mazingira na uchimbaji choo duniani kitaifa na kufanya maonyesho mbalimbali ya usafi wa mazingira na uboreshaji wa vyoo.

Akizungumza na Elimtaa Media afisa afya mkoa wa Njombe Mathias Gambishi alisema kuwa katika halmashauri  zote mkoa wa Njombe zinatimiza kampeni za usafi wa mazingira na uboreshaji wa vyoo na kufanya maonyesho ya wiki ya usafi wa mazingira.

Alisema kuwa katika wiki hiyo kututakuwa na maonyesho mbalimbali ya usafi wa mazingira, unawaji na utumiaji bora wa Choo pamoja na uchimbaji wa vyoo.

Alisema kuwa wiki hiyo inaanza Novemba 13 na kufikia kilele Novemba 19 mwaka huu katika halmashauri ya Mji wa Njombe ambapo kila halmashauri itakuwa na maonyesho katika sehemu hiyo ambayo maadhimisho hayo yatafanyika.

Gambishi alisema kuwa wananchi wanakaribishwa katika maadhimisho hayo ambayo yatakuwa na elimu kutoka kwa taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali (NGO) na kuwa wananchi watajifunza ujimbaji wa choo bora kwaajili ya afya za jamii.

Alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuwa na vyoo bora na kutumia maji yanato tiririka katika vyoo vyao na sabuni ili kuhakikisha kuwa ananawa bila kuondoka na uchafu.

Alisema kuwa idara ya afya mkoa wa Njombe inapata changamoto mbalimbali za kuhakikisha kuwa inawafikia wananchi moja kwa moja wakati wa kampeni za afya na usafi wa mazingira ambapo mkoa wa halmashauri zote zinaendesha kampeni hizo.

Alisema kuwa moja ya changamoto kubwa ni kuto kuwa na magari ya kuwawezesha kufanya kwa umakini kampeni zao za kuhimiza wananchi kuwa vyoo imara, na ambao hawana kuvichimba.

"Licha ya kuwapo kwa changamoto hiyo ya ukosefu wa Magari kuna changamoto iliyokuwepo wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wanasiasa walikuwa wanapotosha wananchi kwa kuwaambia kuwa wanatakiwa kuchimbiwa na serikali, baada ya kumalizika kwa kipindi cha uchaguzi wananchi wanauelewa baada ya kuendeleana kampeni zetu za usafu," alisema Gambishi.

Alisema kuwa katika kampeni hiyo wanashirikiana na mamlaka za maji kuhakikisha kuwa wananchi wanaimalisha usafi wa vyoo vyai ili kuto athili mazingira ya vyanzo vya maji na kusababisha kuwa magonjwa ya

"Tunashirikiana na watu wa maji kwa kuwa vyanzo vya maji vikichafuliwa kwa sababu ya watu wanao jisaidia mapolini, kutokana na kuto kuwa na vyoo tutapata magonjwa mbali mbali ya Minyoo na mengine yanayo tokana na uchafuzi wa mazingira," alisema Gambishi.

Aliongeza kuwa maadhimisho hayo yamepelekwa katika mkoa huo kutokana na mkuoa huo halmashauri zake kufanya vizuri katika usafi wa mazingira kutaifa.