JESHI
la Polisi mkoani njombe linawashikilia watu 15 kwa tuhuma za kujiandikisha mara
mbili katika daftari la kudumu la mpigakura kwa mfumo wa Biometric Votar Regstrestion
(BVR) akiwemo afisa wa tume ya kupambana na Rushwa Tanzania Takukuru wa
wilayani Ludewa.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya kukamilika kwa semina kwa Askari Police,
Magereza na Mgamo wa wilaya ya Njombe kamanda wa polisi mkoa wa Njombe, Wilbroad
Mtafungwa (Pichani) alisema kuwa jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watu 15 walio
jiandikisha mara mbili mkoani huo na kuwa linaendelea na msako wa watu wengine
ambao walijiandikisha marambili.
Alisema
kuwa kati ya watu hao kuna baadhi yao wamepandishwa mahakamani katika mahakama
za wilaya zao na kuwa mmoja kati ya walio pandishwa mahakamani amekubali kosa
na kulipa faini ya shilingi laki moja (100,000).
Alimtaja
mshitakiwa aliye kili kutenda kosa hiyo kuwa ni Awatich Sanga mkazi wa Mfumbi
Makete, alifikishwa mahakanani na kukubari kosa na kutozwa faini ya shilingi
laki moja,(100,000) wengine bado kufikishwa mahakanani kutokana na upelelezi kuwa
haujakamilika.
Alisema
kuwa kati ya walio kamatwa kunamfanyakazi wa Takukuru ambaye naye amekamatwa
kwa tuhuma za kujiandikisha marambili ambaye alitambulika kwa jina la Abdul
Badenga mkazi wa Manda Ludewa na kuwa atafikisha mahhakamani upelelezi utakapo
kamilika.
Mtafungwa
aliwataja watu wengine walio kamatwa kwa tuhuma hizo kuwa ni Esta Mgimba, John Mlingo,
wote wakazi wa Ramadhani Walda Mahegema mkazi wa Chaugingi, Bonfasi Mwalongo,
Christina Sange, Adgia Ngwazi, Esta Mhando, Samson Mgaya, wakazi wa wilaya ya Wangingombe, Helena
mpanmgala Saulo Haule, Maria Chaula Jonasan Haule na kuwa huyu amefikishwa
mahakanani.
Aliongeza
kuwa katika wilaya ya Makambako alikamatwa mtu mmoja Jeska Chenana, alisem
akuwa wengine wanaedelea kutafuwa ili kujibu mashitaka yanayo wakabili hasa ya
kujiandikisha marambili.
Hata
hivyo walio baki kufikishwa mahakamani bado upelelezi wa jeshi hilo unaendelea
ili kujibu tuhuma zinazo wakabili watu hao.