Baadhi ya Wakazi wa mkoani njombe hawaifahamu sheria ya mtandao


BAADHI ya wananchi na watumiaji wa mitandao ya kijamii Mkoani Njombe wamesema kuwa sheria ya mitandaoni inayoanza kutumika Septemba Mosi mwaka serikali ilitakiwa kuielimisha jamii hiyo juu ya madhara ya sheria hiyo.

Wakizungumza na kituo hiki walisema kuwa elimu juu ya sheria hiyo haija wafikia na kuwa mpaka inaanza kutumika hawaelewi ni mambo gani yanatakiwa kufanya na mabo gani hayatakiwi kufanywa katika mitandao ya kijamii.

Mmoja wa wakazi wa Mkoani Njombe Math Sanga alisema kuwa anaishangaa sheria hiyo alivyo ielewa kuwa mtu akipokea picha anashitakiwa na aliyeituma.

Hata hivyo baadhi ya wakazi wa Mkoani humo wameiomba elimu ingetolewa kwaza kabla ya kuaza kutumika na kuwa wanawasiwasi wa sheria hiyo kuja kwaajili maalumu ya kuwabana watu wa upande fulani na kuwaachia watu fulani.


Baraka Tave na Anjelo Mgaya wanasema kuwa wanashauri sheria hiyo elimu ipite kwanza kwa jamii wanayo ipelekea sheria hiyo.