WAKATI tume ya taifa ya uchaguzi NEC ikisimamia msimamo wa
wananchi kuondoka eneo la kupigia kura baada ya kupiga kura baadhi ya vyama vya
siasa vimesimamia msimamo wa kulinda kura kwa kukaa mita 200 kwa mujibu wa
sheria baada ya kupiga kura.
Msimamo huo umetolewa juzi, Mjini Njombe na mgombea ubunge
wa jimbo la Njombe kusini, Emmanuel Masonga, (Pichani) katika wa mkutano wa wadau na
waandishi wa habari, ulioandaliwa na
chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe (Njombe Press Club NPC).
Masonga alisema kuwa watafanya hivyo kwa mujibu wa sheria na
kuwa wanaendelea kutoa elimu kwa wapigakura kutoleta vurugu wakati wa kulinda
Kura na kusubili matokeo ya uchaguzi wakiwa umbari unao kubarika kisheria.
Alisema kuwa kunawanasiasa wanao wadanganya wananchi kuto
linda kura zao na kuwataka wanasiasa hao waielewe sheria hiyo na kuwa wao
watafuata sheria.
Alisema kuwa hawata kubari upotoshwaji wa kuwa baada ya
kupiga kura waende kulala kitu ambacho hakita wezekana na kuwa wapige kura na
kuzilinda, na kuongeza kuwa haita wezekana kura kuziacha zikaibiwa.
Kwa upande wa mratibu wa uchaguzi mkoa wa Njombe, Herial
Danda, alisema kuwa sheria ya uchaguzi kuhusu kulinda kura zipo mbili ambazo
kama kutatokea vurugu zitambana mwananchi kwa kuwa zipo mbili tofauti na kusema
kuwa wananchi ni bora wakarudi nyumbani kusubiri matokeo.
Alisema kuwa sheria ya serikali za mitaa ya uchaguzi inasema
kuwa mpiga kura anatakiwa kukaa umbari wa mita 300 akilinda kura na sheria ya
uchaguzi inamtaka mpiga kura kukaa mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura
kulinda kura.
Alisema kuwa mtu akikamatwa kwa kosa la kuwa eneo la kupigia
kura atahukumiwa kwa sheria zote mbili na mahakama haita angalia ni seria ipi
hivyo wananchi wajiadhali kwa hilo kwani wanaweza wakawa umbari wa mita 200
ikatumika sheria ya umbali wa mita 300 wakajikuta wapo hatiani.
Aliongeza kuwa waandishi wa habari wataruhusiwa kuingia
katika vituo vya kupigia kura na kutoa rai kwa waandishi wa habari kuvaa
vitambulisho vyao.