WAKATI serikali ikisema elimu bure kuanzia mwaka ujao mkuu
wa shule ya msingi Matiganjola ya halmashauli ya wilaya ya Njombe, iliyo shika
nafasi ya 48 kati ya shule 49 za wilaya amewatrudisha wanafunzi nyumbani
kufuata mahidi kwaajili ya chakula cha mwaka 2016.
Wakizungumza kwa jaziba baadhi ya wazazi wa watoto
waliorudishwa nyumbani na y wa shule hiyo, Athanasio Ulime, walisema kuwa
wameshangaa kuona kuwa watoto wao wanarudishwa michango wakti michango ya
chakula kwa mwaka huu inatosha na kukubaliana kupeleka michango wanapo mpeleka mtoto
mwezi wa kwanza.
Mmoja wa wazazi Amina Kihwele alisema kuwa ameshangazwa na
kitendo cha mkuu wa shule anayo soma mtoto wake kuona anawafukuza watoto
kwaajili ya michango ya mwaka ujao wakati mwaka huu haujaisha.
Aliongeza kuwa shule hiyo imefanya vibaya kutokan ana watoto
kurudishwa nyumbani mbara kwa mara kufuata michango na kuwa mwaka huu shule
hiyo imfanya vibaya na kufaurisha watoto watatu pekee.
Wazazi wengine walitilia shaka kukusanywa kwa michango hiyo
ikiwemo ya mahindi, kwa kusema kuwa waalimu wanataka kufanya chakula chao,
kauli hiyo inapinga na kauli ya mkuu wa shule hiyo.
Mkuu wa shule hiyo alisema kuwa siku ya juzi watoto
walifukuzwa shule asubuhi kwa lengo la kwenda kuwakumbusha wazazi wao michango
muda wa asubuhi badala ya kwenda kufanya mazoezi ya mchaka mchaka.
Ulime alisema kuwa alifanya hivyo kuchukua michango ya
chakula kwa kuwa wanafunzi 480 katika
shule hiyo bado hawajachangia hivyo muda wa mchaka mchaka akaona ni vyema
wakafuatilia michango hiyo.
Aliongeza kuwa wakati wanafunzi wameondoka kwa wingi
aliendelea na kikao katika ofisi yake na baadhi ya viongozi wa shule hiyo.
“Wanafunzi wengi hawajatoa michango ni wanafunzi zaidi ya 480
nikaona mda wa nusu saa wakati waende kuchukua michango na kurudi, kwa kuwa
nimeona kama chakucha kimepungua,” alisema Ulime.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi
Matiganjora Jactan Mwani akizungumzia
swala la kuwarudisha wanafunzi nyumbani kwa kosa la wazazi kushindwa kupeleka
michango ya chakula shuleni amesema
swala hilo walikubaliana kwenye mkutano wa hadhara wa Octoba 13 huku
akisema wananchi wanaendekeza siasa hata muda ambao siasa zimekwisha.
“Suala la wanafunzi kurudishwa nyumbani ni suala ambalo
tulikubaliana na wazazi katika mkutano wa hadhara lakini wazazi wamekuwa
wakiendeleza siasa hata muda ambazo sio wa siasa,” alisema Mwani.
Baadhi ya wanafunzi waliorudishwa nyumbani walisema kuwa
wamereudishwa nyumbani kwa kukosa michango
huku bwanafunzi wengine wakiendelea na masomo kama kawaida.
Aidha Afisa elimu shule za msingi halimashauli ya wilaya ya
Njombe Catherine Kiaule alisema kuwa taratibu za elimu mkuu wa shule haruhusiwi
kumfukuza mwanafunzi kwa kosa za Mzazi wake kwa kuwa kitendo hicho kinaathili
elimu ya mtoto.
Alisema kuwa mwalimu
mkuu wa shule anatakuwa kuchukua hatua ya kupeleka jina la mzazi ambaye halipi
michango kwa wakati kwa mtendaji wa kijiji ili kushughilikia kama anaonyesha
kuto tii hatua za kisheria kuchukuliwa dhidiyake lakini sio kwa kidendo kilicho
fanywa na mkuu huyo.
Alisema kuwa hatua ambayo ofisi yake itachukua ni kumshauri
mkuu hiyo na kutoa ushauri kwa wazazi hukakikisha kuwa watatoa michango kwa
wakati.
Kufuatia kufukuzwa kwa wanafunzi na kurudi nyumba wazazi wa
kijiji hicho waliandamana kupinga hatua hiyo ya walimu kuwafukuza watoto wao
shuleni na kuacha masomo, shule hiyo imeshika nafasi ya 48 kati ya shule 49 za
halmashauli hiyo ya Njombe kitu kinacho daiwa na wazazi ni watoto kurudishwa
nyumbani na waalimu kisa kukosa mazomo.