OFISI YA MTAA WA GWIVAHA YAVUNJWA


WANANCHI wa mtaa wa Gwivaha mjini Njombe wameilalamikia halmashauri kubomoa ofisi yao ambayo inadaiwa na halmashauri hiyo kugeuza kuwa stendi ya Gari aina ya Noah kwa muda ili kuongeza mapato.

wakizungumza kabla ya kuvunjwa kwa ofisi yaokwa nyakati tofauti wananchi na badhi ya viongozi wa mtaa huo wamesema kuwa haiwezekani kuondolewa ofisi yao pamoja na kituo cha kujifunzia watoto wadogo (Chekechea).


Mwenyekiti wa mtaa huo Denis Malekela alisema kuwa ofisi hiyo haita wezekana kubomolewa kwa kuwa wananchi wa mtaa huo hawana taarifa yoyote kuhusiana na kubomolewa kwa ofisi hiyo na kuwa hawata hama katika eneo hiyo kwa kuwa lilianzishwa na waasisi wa taifa hili pamoja na wazee wao.

Alisema kuwa miaka ya nyuma jengo hilo lilijengwa kwaajili ya ofisi za kijiji pamoja na kituo cha chekechea kwa watoto wadogo wa kijiji wakati huo huku mitaa yote ya Njombe mjini ikizaliwa kutoka katika mtaa huo.

Bada ya kuvunjwa kwa ofisi hiyo Mwenyekiti wa mtaa huo alisema kuwa ofisi yao imevunjwa kukiwa na baadhi ya makablasha yaliyo kuwa na kumbukumbu za muhimu pamoja na kesi za wakazi wa mtaa huo.

Alisema kuwa suala hilo amelifikisha katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Njombe na kuwa ofisi ya mkoa imeshangazwa na kitendo hicho.

Mwannchi wa mtaa huo wakizungumza kabla kuvunjwa Bahati Luvela alisema kuwa wananchi wa mtaa huo hawana taarifa yoyote kuhusiana na kuwapo kwa kubadilishwa kwa matumizi ya eneo hiyo la chekechea na ofisi ya mtaa.

Alisema kuwa wameshangaa asubuhi kuona kuwa kuna katapola ambalo tayari kwaajili ya kubomoa jengo la ofisi hiyo kitu ambacho kimewashitua na kuwa hawajaambiwa wapi kwa kwenda.

Aidha baadhi ya wajumbe wa mta huo wamesema kuwa hakuna kikao chochote kilicho kaliwa na uongozi wa mta huo kwaajili ya kubadilisha matumizi ya eneo la ofisi za mtaa wao.

Andoya Mgaya ni moja wa wajumbe wa mtaa huo amesema kuwa kubombolewa kwa ofisi hiyo kutasababisha usumbufu kwa watoto waliotakiwa kusoma hapo pamoja na wananchi walio kuwa wakipata huduma hapo na kuwa taarifa za ubomoaji hazijawafikia.


"Mkurugenzi ameamua kututengenezea matatizo lakini na sisi tutahakikisha anapata matatatizo kwa kuwa haiwezekani ofisi ikavunjwa bila ya wananchi kujulishwa, tuenda mahakamani ili kuandaa stop oda kwaajili ya kuzuia kubomolewa kwa ofisi yetu," alisema Benedicto Chapwila mjumbe.

Alisema kuwa mkurugenzi anashinikizwa na baadhi ya viongozi kufanya ubomoaji wa eneo hiyo na hawata kubari eneo la kusomea watoto wao kuwa eneo la kupaki magari aina ya Noah.

Hata hiyo msimamo wa halmashauri wa kubomoa jengo hiyo unatolewa na mwenyekiti wa halmashauri ya mji njombe Edwin Mwanzianga ambaye anasema kuwa mtaa hauna jengo la ofisi na majengo yote yapo chini ya halmashauri.

Kabla ya kuvunjwa alisema kuwa eneo hilo linavyunjwa na kutakuwa na eneo la maegesho ya noah ambazo zinatoka vijijini kutokana na noa hizo kuto kuwa na eneo la kupaki wakati wakiendelea na ujenzi wa stendi mpya ambayo itakuw ana nafasi ya kutosha.


Alisema kuwa taarifa za wapi inahamia ofisi hiyo afisa mtendaji wa mtaa huo anajua itakapo kuwepo na kuwa sasa inahamia pale ilipo kuwa ofisi yao zamani maeneo ya Ujenzi umbali wa kilomita moja na nusu hadi mbili kutoka katikati ya mtaa huo wa Gwivaha.


Aidha ofisi hiyo imevunjwa na kusawazishwa eneo hilo kwaajili ya kupaki gari aina ya noah ambazo halmashauri imedhamilia kuzipaki katika eneo hilo ambalo lilikuwa ni ofisi za mta na kituo cha chekechea.

Inadaiwa kuwa ni mgogoro wa kisiasa unao sukumwa na halmashauri kusababisha eneo hilo kuvunjwa kwa kuwa mwenyekiti wa chama cha upenzani ndio alipika katika uchaguzi wa wenyeviti wa mitaa wa disema mwaka 2014 kitu kitakacho wanyima wananchi kuendelea kupata huduma eneo la mtaani kwao.

Bila kujali ofisi hiyo ilikuwa na ilikuw ana dokomenti za muhimu kama kesi za watu na thamani za ndani vyote vinadaiwa kuzamia katika kifusi cha tofari baada ya kuvunjwa kwa ofisi hiyo.