MKUU wa mkoa wa Njombe, Dkt Rehema Nchimbi, amewataka wakuu wa wilaya za mkoa huo kuhakikisha kuwa wanawafuatilia wakuu wa idara katika Halmashauri zao wanao fanya siasa na mda wa kazi kwani wanaiibia serikali mdawake.
Wito huo ameutoa wishoni mwa wiki iliyopita wakati akimwapisha mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe, Dkt. Asunta Mshama, ambaye alikuwa ni mbunge wa jimbo la Mkenge mkoani Kagera na kushindwa katika kura za maoni kabla ya kuteuliwa na raisi kuwa mkuu wa wilaya.
Dkt. Nchimbi alisema kuwa anataarifa za wakuu wa idara ambao wanajihusisa na siasa na kuacha majukumu yao na kuto fanya kazi walizo ziomba wakati wanatafuta ajira.
Alisema kuwa wakuu wa idala wamekuwa wakiikosea serikali kwa kuwa wamekuwa wakiibia muda na kmwenda kupiga kampeni kwa vyama wanavyo vijua wao na wanajidanganya itapita na wameahidiwa ukuu wa wilaya ya ukuu wa mkoa.
“Wote mliomo humu wengi mpo hicho chama kingine na mmeahidiwa ukuu wa wilaya baada ya kuingia, na ` mnalipwa na serikali hii na mnafanya kazi za kampeni wakati ambao mlitakiwa kuutumikia umma wa watanzania ambao mliandika mkataba wa kuwatumikia, na mwishi wa mwezi mnachukua mshahara,” alisema Dkt. Nchimbi.
Alisema kuwa watumishi hao akiwabaini hatakama hana uwezo wa kuwafuta kazi lakini akiwabaini waziwazi atajua chakufanya.
Hivyo aliwataka wakuu wa wilaya wote mkoa huo kuhakikisha kuwa wanafuatilia watumishi hao wanaoiibia serikali muda wake na kufanya kampeni katika chama hicho kingine na kuahidiwa ukuu wa wilaya na wamtumie majina.
Aidha alitoa ufafanuzi wa wakuu wa wilaya walioteuliwa wakati huu na uvumi unao sema kuwa ni wakuu wa wilaya wa uchaguzi alisema kuwa serikali haina liziko na haiwezekani wilaya ikakaa bila kuwa na mkuu wa wilaya kwa muda mrefu.
Alisema ndio maana serikali imeteua wakuu wa wilaya kwa wilaya ambazo hazina wakuu wa wilaya tu na kuwa uteuzi huo haina uhusiano wowote na siasa na kuwa wasipo teuliwa kipindi hiki wilaya inaweza kukaa miezi zaidi ya minne bila ya kuwa na mkuu wa wilaya.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya huyo Dkt. Mshama akila kiapo alisema kuwa atakuwa mtiifu kwa serikali kuwa atafuatilia wale wote wanaoonekana kuwa wanafanya siasa muda wa kazi na kuhakikisha umma unapata huduma zao walizo zitarajia kuzipata wakiingia katika ofisi za umama.