Wafugaji njombe kuelimishwa ufugaji wa kisasa

WAFUGAJI wa ng’ombe mkoani Njombe wamepewa changamoto kufanya ufugaji kilimo kibiashara ili kuongeza uzalishaji na ubora wa maziwa utakaoweza kuinua kipato chao imeelezwa mkoani humo jana.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji ya Mfuko Kichocheo wa Kilimo Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT CTF), Dr Rosebud Kurwijila, wakati akizungumza na baadhi ya wafugaji wa mkoa huo kwenye semina ya siku tano ya Kilimo Ufugaji Biashara (FAAB)  iliyoandaliwa na SAGCOT CTF kwa kushirikiana na Kiwanda cha Maziwa Njombe pamoja na  Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara, (UNCTAD ikiwa na lengo la kuinua kipato  kutokana na ufugaji wa ng’ombe wa maziwa kibiashara.  

Alisema hii ni semina ya nne kutolewa nchini Tanzania kwa uratibu wa Mfuko wa SAGCOT CTF  na UNCTAD mara ya kwanza ikiwa ni mkoani Tanga 2015 mafunzo yakitolewa kwa awamu tatu yakiwa na madhumuni ya kuwafanya wafugaji wakulima wanaondokana na kilimo cha kujikimu.  

“Mfuko Kichocheo wa SAGCOT CTF unatoa ufadhili kwa wafugaji hao kupitia kiwanda cha kusindika maziwa cha Njombe ambapo mfuko ulifanya utafiti wa kujua nini mfugaji anahitaji kuinuka kiuchumi,” alisema.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa SAGCOT CTF, John Kyaruzi amesema kuwa sasa ni wakati wa wafugaji kutajirika kutokana na ufugaji na ndio maana ufadhili wa elimu hiyo utasaidia wafugaji kufuga kibiashara ambapo mahitaji makubwa ni kupata  ng’ombe mwenye uwezo wa kutoa maziwa kwa wingi.

“Wafugaji wengi wapo vizuri katika hatua ya kulisha mifugo yao lakini wanachokikosa ni elimu ya uchaguzi wa ng’ombe wazuri wa maziwa na hivyo Mfuko Kichocheo wa SAGCOT CTF  hautatoa mkopo wa pesa pekee kwa wakulima bali kuwawezesha kutoka na kile mfugaji atakacho,” alisema.


Katibu Mtendaji huyo wa SAGCOT CTF aliongeza kuwa elimu hiyo ni muhimu kwani itasaidia wakulima wafugaji kutambua kuwa kilimo ni biashara huku pia wakipewa mbinu ya kupunguza gharama katika ufugaji wa ngo’mbe wa maziwa kibiashara na kwa matumizi yao hivyo kukuza uchumi wa mkulima mmoja mmoja,  jamii na pia kujenga afya zao kutokana na kutumia maziwa bora.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Iluminata Mwenda alisema kuwa wafugaji hao watumie vizuri fursa hiyo kwa kuwa wanaletewa elimu ya kuwa na uchumi mzuri na kuwa wafugaji wakifanya vizuri halmashauri nayo itaongeza kipato chake kwa kuwa na kiwanda cha maziwa kinachozalisha kwa wingi.

Nao baadhi ya wafugaji wameishukuru SAGCOT CTF, UNCTAD pamoja na washirika wengine waliofanikisha semina hiyo kwani kupitia mafunzo hayo wanaweza kuwa ufugaji wenye tija kwa ajili ya kuinua kipato na kuboresha afya zao.


Mfuko wa SAGCOT CTF ulianzishwa Mei 2011 chini ya sheria ya wadhamini ya Mwaka 2002 chini ya Mpango Shirikishi wa Uchumi nchini (PPP), kuchochea maendeleo katika sekta ya kilimo nchini. Katika kufikia malengo mfuko ulitafuta wabia muhimu kufikia azma hiyo hivyo Shirika la UNCTAD ni mshirika wake katika kutoa utaalamu elekezi. (technical assistance)

Mratubu wa biashara wa Mfuko Kichocheo SAGCOT, Abdala Msambachi   akitoa ekelimu kwa wagugaji wa ng’ombe wa maziwa mkoani Njombe ili kufanya ufugajiwa kisasa na uinua uchumiwao elimu hiyo inayo tolewa na Mfuko Kichocheo SAGCOT.