Imeelezwa Kuwa Migogoro Ndani ya Vyama Vya Waandishi wa Habari Nchini Pamoja na Nidhamu Mbaya ya Matumizi ya Fedha ni Chanzo Cha Mifarakano na Kuvunjika Kwa Vyama Hivyo.
Kauli Hiyo Imetolewa na Mjumbe wa Bodi ya Umoja wa Vilabu Vya Waandishi wa Habari Tanzania UTPC Deogratias Nsokolo Ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Kigoma Wakati Akizungumza na Wanachama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Njombe.
Akiwa Katika Ziara na Baadhi ya Viongozi wa Chama Cha Waandishi wa Habari Kigoma Mjumbe Huyo Amesema Kwa Kuwa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Njombe Bado ni Kichanga ni Vyema Nidhamu ya Matumizi ya Fedha Zitakazo Kuwa Zinaletwa na UTPC Zikatumika Vizuri Ili Kuwanufaisha Wanachama Wote Katika Kufikisha Ujumbe Kwa Jamii Juu ya Changamoto Zinazowakabili.
Aidha Nsokolo Amesema Kuwa Uwepo wa Chama Cha Waandishi Habari Katika Mkoa wa Njombe Kutasaidia Kuleta Maendeleo Katika Mkoa na Kupunguza Matatizo Yaliyopo Katika Jamii.
Mwajabu Kigaza Hoza ni Mtunza Hazina Katika Chama Cha Waandishi wa Habari Kigoma[KGPC]Ambaye Ameutaka Uongozi wa Chama Cha NPC Kutenda Haki Katika Uteuzi wa Wanahabari Watakaotakiwa Kupatiwa Mafunzo Ili Kuwawezesha Kujifunza Namna Ya Kujengewa Uwezo.
Akizungumza Kwa Niaba ya Katibu Mtendaji wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Njombe NPC,Mjumbe wa Kamati Tendaji ya NPC Bwana Michael Katona Amepongeza Hatua ya UTPC Kutambua Uwepo wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Njombe na Kukitembelea Huku Akiomba Kutolewa Kwa Mafunzo ya Mara Kwa Mara Kwa Wanahabari Juu ya Kwenda na Wakati Katika Tasnia ya Habari.
Hata Hivyo Katika Kufanikisha Hayo Yote na Kurahisisha Utendaji Kazi Kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Njombe UTPC Inatarajia Kuleta Vifaa Kwa ajili ya Kuwasaidia Wanahabari Katika Kazi Zao.