KANISA la kiinjili la kirutheli Tanzania mkoani Njombe limefungua zawadi za boxing day na watoto 123, waishio katika mazingila magunu na Chokolaa, kwa kuwapa mashuka, masweta, na kula chakula pamoja cha mchana na jioni kwa Chokolaa, zawadi zikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi, milioni 3.6 na kuwafa fulsa watoto hao kueleza changamoto zao kwa mkuu wa mkoa.
Ibada hiyo iliyo andaliwa na Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Kusini kanisa la KKKT, Isaya Mengele, ikiwa na mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Njombe Dr Rehema Nchimbi ilihusisha watoto wanao ishi kwa kula majalalani 18 na watoto tatima ambao wanaishi na ndugu zao kutoka shule za msingi 105 na kufikia jumla ya watoto 123 walio huzulia ibada hiyo na kanisa likiwa limelenga watoto 150 kusaidiwa.
Akikabidhi zawadi za masweta, branketi, t-shirt na kofia zawadi zilizo kuwa zimeandaliwa na Askofu Mengele zilizokuwa na dhamani ya milioni 3.67 mkuu wa mkoa Dr. Nchimbi alisema kuwa watoto hao wanahitaji msaada mkubwa kutoka kwa jamii ili kuondokana na maisha magumu wanayo ishi.
Alisema katika makanisa na misikiti kuna waumini wenye pesa nyingi, na wanazitumia vibaya kwa kutumia katika anasa na wengine kulalia pesa wakati kuna watu wanaishi katika mazingira magumu na wanashindwa hata kupata mlo mmoja.
Dr. Nchimbi alipongeza juhudi za kanisa hilo kuangalia watoto hao waishio katika masingira magumu na kula nao chakula pamoja na msaada huo unasaidia kuonyesha watoto hao kuwa kuna watu wanao wajali na kuwapa furaha na kuwasaidia kulala usinguzi mzuri.
“Kanisa mmefanya kiti kukubwa kuliko kawaida kwani hawa ni watopto ambao ni taifa la kisho na msaada huu mtawawezesha kuishi na kulala usingizi mzuri,” alisema
Awali wakizoma risala yao watoto hao mbele ya mkuu wa mkoa na askofu walisema kuwa wamekuwa wakilala katika mabanda ya masiko mkoani Njombe ambapo wamekuwa wakinyanyashwa na walinzi kwa kufukuzwa wakiwa wamelala na mara nyingine kufanyishwa mazoezi usiku kucha mda ambao ilipashwa kuwa wamelala.
Msoma risala hilo Danford Mrigo alisema kuwa wamekuwa wakilalia maboksi, kuvaa nguo za kuokota, na kula matunda yaliyo tupwa majalalani huku wakijishugulisha na shuguli za kubeba mizingo licha ya kukumbana na changamoto ya kuhisiwa wizi kiti kinacho sababisha kukosa kazi zao zinazo waingizia kipato.
Risala hiyo ilimuinua askofu Mengele na kuitaka serikali kuangalia uwezekano wa kuwapatia watoto hao mahali pa kulala usiku kwani nao watoto hao ni moja ya watu wake ambao inawaongoza na kuwageukia wararushwa na mafisadi mbalimbali wakiwemo wa Escrow kuachana na tabia hizo na kuwaangalia watoto wanao ishi katika mazingira magumu kama hayo.
Alisema kuwa watoto hao ni wa serikali kwani wao hawajapenda kuishi katika mazingira hayo magumu kwani baadhi yao hawana wazazi na wengine wanawazazi wao lakini wametelekezwa hiyo serikali ianfalie uwezekani wa kuwareshesha watoto hao kwa wazazi wao kwa kuwapatanisha na wambao hawana wazazi kuangalia uwezekano wa kuwasaidia.
Askofu mengele alisema kuwa kanisa hilo kwa siku ya Boxing Day ilimekuwa likijuhusisha na kukaa na watu wenye uhitaji na ndio kitu kilicho lishukuma kanisa hilo kuwatazama watoto hao ambao wamekuwa wakipitia maisha magumu ya kula majalalani na kula nao chakula cha pamoja.
Watoto hao walipatiwa kila mmoja Blanket moja, Sweta, T-shirt, na kofia pamoja na kula chakula cha mchana na Askofu wakiwa na mkuu wa mkoa na watoto chokolaa kula chakula cha usiku kanisani hapo kabla ya kuelekea mahali wanapo lala.
Akifunga ibada hiyo mkuu wa mkoa aliwataka maafisa vijana kuhakikisha watoto hao wanaibuliwa vipaji vyao na kutafutia namna ya kuwasaidia na kuona watoto hao ndio wanapewa kipaumbele katika shughuli mbalimbali kutoa burudani.
Hivyo maafisa vijana kuanza kazi ya kusaka vipaji vya watoto hao ili kuviibua na kuwasaidia kufikia malingo na kwa waled ambao bado hawajaenda shule kuwapeleka shule ili kutimiza ndoto zao.
Kwa upande wa watoto hao waliopata zawadi, walilishukuru kanisa hilo na kutoa wito kwa watu wenye pesa kuacha matumizi mabaya ya pesa katyika anasa za kunywaji wa pombe na kuhonga wanawake.
Mtoto George Mwanyika kutokea Ludewa na kuja mjini kutafuta maisha, aliiomba serikali kumsaidia kwenda shule na kutoa wito kwa matajili kujitoa kwa watoto wa aina hiyo na kuomba serikali kuwatafutia sehemu ya kulana na kuwa wamechoka kulala katika mabanda na kuwa nanaumwa na mbu usiku kucha.
Licha ya watoto wengi wanao ishi katika mabanda kufiwa na baba na mama zao lakini ni tofauti kwa mtoto Josphat Msigala ambaye wazazi wake wapo lakini walimtelekeza mjini Njombe na mpaka sasa haelewi wako wapi, alisema kuwa wamekuwa wakikutana na changamoto za kupigwa na walizi hasa wakiwa wamelala.
Alisema kuwa miili yao imekomaa kutokana na mazoeli ambayo wamekuwa wakifanyishwa na walizi na kuwa wamekuwa waiitwa sugu kutokan ana mazoezi hayo, na alitoa shukrani kwa kanisa kwa kuwaona na kuwapatia msaada huo.
“Tumekuwa kutikeshwa na walizi usiku kwa kufanyishwa mazoezi kuzinguka stendi ya mabasi usiku na kupigishwa pushap bila kuwa na makosa yoyote, wito wangu kwa watu wenyepesa kutuangalia sisi kwa kutupatia msaada na kuachana na kufanya anasa hasa za kunywa pombe kupindukia, kuhonga na makahaba,” Alisema Msigala.