Wahitimu wa taaluma ya udaktari wa meno na wauguzi katika chuo cha sayansi ya Afya Bulongwa wilayani Makete wakiingia katika ukumbi wa sherehe za mahafari ya kuhitimu elimu yao Septemba 5, 2015
Burudai kidogo ilifanyika babla ya mambo mengine kuendelea
Waziri wa habari na michezo (Mwenye Nyekundu) katika chuo cha Bulongwa
Maabara ya kujifunza kwa vitendo
Muhitimu kwa masomo ya udaktari wa meno akizunhumza na waandishi wahabari (hapapo pichani)
Wanachuo wakiwa katika ukumbi wa sherehe za maafari ya kuhitimu elimu yao ya uuguzi na utaktari wa meno chuo cha Bulongwa Makete Mkoani Njombe
Baadhi ya wazazi na ndugu za wahitimu walio kuja kusheherekea na nduguzao
Mkuu wa chuo cha Bulongwa John Matala akizungumza na wahitimu
Dmo wa wilaya ya Makete Mkoani Njombe
Mgeni Rasmi Prof. Norman Sigalla (Kushoto) akikaribishwa na Mwakilishi wa askofu wa KKKT-Makete
Wahitimu wakisoma Lisala mbele ya Ngeni Rasm
Wahitimu wakila kiapo cha kuuhakikishia uma kuwa watafanya kazi kwa utii na kufuata kanuni za utumishi wa taalkuma yao.
Mwakilishi wa askofu wakitoa neno kwa wahitimi hao
Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Songea na mgombea ubunge jimbo la Makete mkoani Njombe na mgeni rasimi katika Maafari hayo ya wahitimu wa Uuguzi na udaktari wa meno katika Chuo cha Bulongwa.
MC katika maafari hayo Sanga akiendesha shuguli hiyo
VITENDO vya Rushwa maneno machafu kwa baadhi wa watumishi wa hospitali wakiwemo wauguzi na madaktari vimedaiwa kuwa ni hulka ya mtu binafsi na sio maadili wanayofundishwa katika vyuo vya taaluma yao.
Hayo yamebainishwa na baadhi ya wanachuo na wahitimu wa chuo ya Sayansi ya afya Bulongwa cha wilayani Makete Mkoani Njombe, ambao wamesema kuwa vitendo vya Rushwa na Lugha chafu havifundishi chuoni na kuwa wanafundishwa kuwa wataratibu wanapo hudumia wagonjwa.
Mmoja wa wahitimu katika chou hicho Dr. Daniel Ngailo amesema kuwa miaka ya sasa maadili ya taaluma hiyo wamekuwa wakifundishwa na kuwa ndio maana katika vituo vya afya mpaka hospitali vitendo vya maneno machafu vimepungua kutokana na maadili kufundishwa sana.
Hata hivyo Maulisia Mlowe anaye hitimu mafunzo ya uuguzi anasema kuwa vitendo vya rushwa na kashifa kwa wagonywa vinakuwa ni hulka ya mtu binafsi na tamaa huku akisema kuwa serikali iongeze kiwango cha mishahara ili kuhakikisha kuwa wauguzi wanafanya kazi bila kuwa na tamaa ya pesa kutoka kwa magonjwa na kuondoa vitendo vya Rushwa.
Kwa upande wake mkuu wa chuo cha Bulongwa, John Matala amesema kuwa serikali imekuwa ikiwatembelea mara kwa mara na kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa inakuwa bora na kuwa katika chuo hicho wahitimu wanao toka wanaende kuwa wenye maadili kutokana na walivyo wafundisha.
Alisema kuwa chuo hicho wanamalengo ya kuwa chuo kikuu na kuanza kutoa elimu ya afya kwa hadhi ya chuo kikuu, na kuwa wanatarajia kuongeza vitengo vingine vya kutoa wahudumu wa afya.
Naye mgeni rasimi katika maafari hayo aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Songea kwa sasa ni mgombea wa ubunge jimbo la Makete Prof. Norman Sigalla amesema kuwa chuo hicho kinatakiwa kuwa na wakuu wa bodi wenye uwezo wa kifedha na watu wenye ubunifu ili chuo hicho kufikia malengo yake kwa haraka ya kuwa chuo kikuu.
Alisema kuwa kuna watu wenyeuwezo ka kuandaa miradi katika wilaya hiyo na chuo kinatakiwa kuwatumia watu hao ili kiweze kufikia malengo yake mapemba ya kuwa chuo kikuu ya afya kama yalivyo malengo yao.