Siasa za njombe wanachama wa CCM na Chadema wakimbilia ACT

BAADHI ya wakazi wa jimbo la Njombe Kusini wanahamia katika chama cha ACT Wazalendo baada ya kuonekana kuwa kunamisimamo waliyo kuwa wanategemea katika vyama walivyo kuwa wanavitegemea kuwafukusha mahari.

Hayo yamebainishwa hivi karibuni wakati Chama cha ACT Wazalendo kikiendelea kupokea wanachama wakati kampeni zikiendelea na kupokea wanachama zaidi ya 2000 katika mkutano wao wa juzi.

Akizungumza na NIPASHE mkoani Njombe mgombea wa Ubunge jimbo la Njombe Kusini Kupitia chama cha ACT Wazalendo, Emilian Msigwa, alisema kuwa licha ya chama hicho kuwa ni kipya na hakukuwahi kuwa na uongozi wowote watu wanamwitikio na wanajitokeza kwa wingi kujiunga nacho.

Alisema kuwa kutokana na kuwapo kwa migogolo katika vyama ambavyo walikuwa kuona kuna migogoro mingi ambayo wananchi hawakutegemea iwepo na kuwa baada ya kuona mgogoro uliopo katicha chama cha Democrasia na Maendeleo, (Chadema) Taifa wananchi wanahama chama hicho.

Msingwa alisema kuwa wanachama wengi wanao jiunga na chama hicho wanakimia migogoro na kuona kuwa mabadiliko wanayo yataka hayapo Chama Cha Mapinduzi na walitarajia kuyapata Chadema lakini wanaona hayawezikupatikana kutokana na migogoro inayo onekana.

"Wananchi walitegemea kuwa kutakuwa na mabadiliko wanayo taka katika vyama hivyo vigongwe lakini wanao ona kunamigogoro inayo jitokeza baina ya viongozi ka viongozi," Alisema Msingwa na kuongeza.

"Katika chama cha Chadema mkoa wa Njombe kuna migogoro ya Chini chini inaendelea na katika chama cha CCM nako hali sio shali ndani na nje kwa kluwa wananchi wameletewa mtu ambaye hawakumtaka na katika mchakato wa Kampeni ameachiwa mweyewe azifanye," alikazia.


Alisema kuwa wananchi mwitikio wao ni mkubwa kujionga na chama hicho kutokana na kile kilicho fanyika taifa na wakati wa mchakato wa kupata wagombea wa nafasi za ugunge ndipo lilipo anzia tatizo akitokea mtu kutoka kabila fulani hata kama alikuwa watatu anawekwa wa kwanza.

Alisema kuwa mikakati yake baada ya kushinda  atahakikisha vipaumbele vya elimu vinatiliwa mkazo na kuhakikisha kuwa maendeleo yanasonga mbele.

Akizungumzia hali ya kisiasa katika jimbo la Njombe Kusini alisema kuwa wanasiasa wanaogombea jimbo hilo wana lugha chafu wanapokuwa majukwaani huku wenginwe wakikimbiwa na wananchi waliopo katika mkutano.

Hata hivyo baadhi ya viongozi waliokuwa tegegemeo kwa CCM wamehamia chama cha ACT kumuunga mkono mgombea hiyo ambapo chama cha mapindizi ni moja ya pigo kwa kipindi hiki cha uchaguzi.


Mmoja wa wanachama walio kihama chama cha CCM akitangaza uamzi wa kukihama chama hicho Juzi, Evarist Lupenza alisema amechukua uamzi huo kutokana na kutokuwa na imani na mwenendo ulivyo kwa sasa, kwani hakina tena Demokrasia na hakitendi haki kama ilivyokuwa zamani.

Lupenza alisema kwa sasa chama hicho kunaendeshwa kwa chuki, fitina, hila, ubaguzi na majungu.

“Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa sasa kinaendeshwa kwa chuki, hila, ubaguzi, fitina na majungu. Kwa kuwa nina akili timamu nimeona siwezi kuendelea kuwa ndani ya chama kinachoendeshwa kwa mtindo huu, kwa kuwa nitakuwa siwatendei haki watanzania,” alisema Lupenza.

Alisema hakuridhika na mchakato wa kumpata mgombea wa Rais ndani ya chama hicho na Mbunge katika Jimbo la Njombe Kusini.

“Nimeamua kuachia ngazi zangu zote ndani ya CCM na kuihama bila kushawishiwa wala kushinikizwa na mtu yeyote, bali sijaridhika na mwenendo ulivyo kwa sasa ndani ya CCM,” alisema Lupenza na kuongeza.

Alisema kutokana na kukosekana demokrasia ndani ya chama hicho tawala, kimepelekea kupata mgombea wa Ubunge katika Jimbo la Njombe Kusini, Edward Mwalongo, asiyekuwa na ushirikiano, na kwamba kinatumia nguvu kubwa kumnadi kwa kile alicho dai kuwa hakubaliki na jamii.

“Kwenye mchakato wa kumpata mgombea wa Urais ndani ya CCM, wajumbe takribani 28 wa jumuia ya wazazi taifa tulikuwa tunamuunga mkono Lowassa (Edward) lakini baada ya kupatikana mgombea John Magufuli kwa sasa wote tumetengwa, Mwenyekiti wetu taifa Abdalah Bulembo naiendesha jumuia hiyo kama yake binafsi bila kutushirikisha,  hizi zote ni hila, fitina na chuki kwa kuwa tu tulikuwa friends of Lowassa (marafi wa Lowassa),” alisema.

Kabla ya kutangaza kukihama chama hicho, Lupenza alikuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi Taifa, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya na Mkoa wa Njombe, Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Baraza Kuu la Wazazi CCM Mkoa na Wilaya ya Njombe