MBUNGE VITI MAALUMU NJOMBE AUNGANA NA WANANCHU KUZIBA SHIMO KUBWA LILIZO FUNGA BARABARA

WATUMIAJI wa barabara ya nyuma ya uwanja wa ndege wameamua kujitolea kuziba shimo lililokuwepo katika barabara hiyo ambalo lilikuwa likileta ushumbufu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema kuwa wamekunbwa na adha ya kupita katika eneo hilo  kwa muda mrefu hivyo wameamua kujitoa kufanya ukarati wa eneo hilo korofi.

Wamesema kuwa eneo hilo lilikuwa kama limesahaulika na wahusika na kuwa kwa sasa watapita bira kunasa kwa magari na pikipiki zao.


Mmoja wa wananchi hao Emmanuel Mapunda alisema kuwa serikali kuna uzembe iliufanya katika eneo hilo ambalo kulitakiwa kuwekwa kalavati ambalo lingetoa maji kutoka upande mmoja kwenda upade unao fuata.

Alisema kuwa chanzo ya kuharibika kwa barabara hiyo kuwa ni kuwapo kwa maji kujaa kwenyekona na kushindwa sehemu ya kwenda mvua zikinyesha.

Hata hivyo dereva wa bodaboda Lemigiusi Mtewele alisema kuwa barabara hiyo ilikuwa nio kero kubwa kwao kwa kuwa ilikuwa ni sumbufu na kuwa sehemu hiyo imekuwa ikiharibika mara kwa mara kipindi cha mvua.

Alisema kuwa yeye amesha wahi dondoga katika eneo hilo akiwa amebeba mzigo huku wakilazimika kupita katika maeneo ambayo sio barabara.

Mbunge wa viti maalumu mkoa w anjombe Licia Mlowe anaamua kuungana na wananchi hao kuhakikisha kuwa eneo hilo linapitiba na kuhakikisha kuwa mvua zinazo endelea kunyesha haziikati tena barabara hiyo.


“Eneo hilo lilikuwa ni kelo kwa wananchi na tumekungana na wananchi wanaotumia barabara hii na kuanza kuchimba ili kuweba bomba ambalo litakuwa likihamisha maji yaliyo kuwa yakijaa katika kona ya barabara na kusababisha uharibifu,” alisema Mlowe.

Barabara hiyo inaingia katika mitaa ya Nzengelendete nyuma na uwanja wa ndege na kipindi baraabara hiyo imeziba wananchi walilazimika katikati ya uwanja wa ndege kupukana na adha hiyo.