ZAIDI YA Mbwa na paka 70 wameuwawa katika mamlaka ya mji
mdogo wa Rujewa wilayani Mbarali mkoani Mbeya ikiwa ni jitihada za kupambana na
kichaa cha Mbwa kwa wakazi wa halmashauri hiyo.
Mbwa hao na paka wameuwawa wakati kukiendelea na kutolewa kwa
elimu kwa wakazi wa mji huo na kuhakikisha kuwa wananchi wanawachanja mbwa
pamoja na paka wao ili kuto leta magonjwa ya kichaa cha mbwa kwa wakazi.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa kamati ya Ujenzi na uchumi kwenye
baraza la mamlaka ya mji mdogo wa Rujewa Daniel Myuki alisema kuwa jumla ya
mbwa 70 na paka mmoja ameuwawa kwa kupigwa risasi na mlenga shabaha wa mamlaka
hiyo kwa kushirikiana na wataalamu wa idara ya kilimo, na afya.
Myuki alisema kuwa zeozi hilo liliendeshwa kwa siku mbili
ndani ya mitaa ya Ibara Rujewa, Isisi, Uhamira, Ihanga, Igomelo, na Lugelele,
ndani ya mamlaka hiyo huku waklio kuwa wakilengwa ni mbwa na paka wa mitaani na
huku wananchi endelea kupatiwa elimu juu ya kuwachanja mbuwa wao.
Alisema kuwa licha ya kutoaelimu pia amewataka wananchi
kuhakikisha kuwa watatii amri ya kufungulia mbwa nap aka wao majira ya saa 4:00
usiku na kuwafungia majira ya saa 12:00 asubuhi.
Hata hivyo alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuhakikisha kuwa
mbwa na paka wao wanawafungi katika mabanda ama kuwafunga kwa minyororo ili
wasizagae mitaani.
“Wananchi tunaendelea kuwapa elimu juu ya kuwafuga vizuri
mbwa na paka wao na kuwafundisha jinsi ya kuwarisha na madhara ya kuto wapa
chanjo mara kwa mara,” alisema Myuki.
Hata hivyo baadhi ya wajumbe walitaka kujua udadi ya mbwa nap
aka katika mji huo wa ili kufanya tathimini ya mbwa nap aka wangapi watakuwa
wametibiwa na wangapi wabebaki kitu kilicho kuwa ni kigumu kwa kamadi hiyo huku
ikisema kuwa mbwa nap aka wanaongezeka kila kikicha hivyo haiwezekani
kupatikana idadi yake kamili.