KISIMA CHA MAJI CHAKABIDHIWA HOSPITALINI NA TBL



KISIMA cha maji chenye uwezo wa kutoa lita 5000 kwa saa kimekabidhiwa rasm katika Hospitali yenye uwezo wa kutoa huduma kwa wananchi kati ya 50 na 60 elfu wan chi mbili za Tanzania na Zambia.

Kisima hicho kimekabidhiwa katika Hospitali ya Tunduma wilayani Momba  Mkoani Mbeya Jana na kampuni ya Bia Tanzania TBL baada ya kukamilika.

Akikabidhi kisima hicho Afisa uhusiano wa kampuni hiyo Doris Malulu  (PICHANI) alisema kuwa kampuni yale imekuwa ikifanya shughuli ya kurudisha faida kwa wananchi kwa kufanya vitu ambavyo vita wasaidia wananchi kwa ujumla.

Alisema mradi huo ni moja kati ya miradi miwili ya visima inayo tekelezwa  na kampuni hiyo Mkoani Mbeya huku mwingine ukitekelezwa wilayani Ileje Mkoani hapa.

Malulu alisema kuwa mradi huo mpaka kukamilika kwake umeghalimu jumla ya shilingi milion24 na kuwa utaweza kutoa lita 5,000 za maji kwa saa na kumaliza tatizo la maji katika Hospitali ya Tunduma wilayani Momba Mkoani Mbeya.

Kwa upande wake Afisa mipango miji wa mamlaka ya Mji mdogo wa Tunduma, Augustino Ngetwa alisema kuwa mradi huo utamaliza tatizo la maji katika kituo hicho kinacho hudumia watu wengi kwa mwaka na watu wanje ya nchi.

Alisema kuwa mbali ya kukamilika kwa mradi huo wa maji Hospitali hiyo inakabiliwa na uchakavu wa mabomba ya kusambaza maji katika vimba mbalimbali vya Hospitali kutokana na kuto tumika kwa muda mrefu sasa.

Naye Mgeni rasm aliye muwakilisha mkuu wa wilaya katika shuguli hiyo ya upokeaji wa kisima hicho Mkurugenzi wa mamlaka ya mji Mdogo wa Tunduma, Aidan Mwashinga, alisema kuwa mamlaka hiyo itatunza maji hayo na kuwa maji yatakayo baki yatasambazwa kwa wananchi.

Alisema kuwa mradi huo utatoa huduma mzuri katika nchi zote mbili na kuwa wananchi waishio mpakani kutoka mchini Zambia watakimbilia katika Hospitali hiyo na kuwa wataisifu kuwa hospitali ya Tundima Tanzania inatoa huduma nzuri na kukuza uchumi wa wananchi jirani kwa kufanya biashara kwa wananchi wa maeneo karibu na hospitali.

Alisema kuwa kutokana na maji kuwa adimu katika halmashauri hiyo wata lina mradi huo na kuhakikisha wananufaika na maji hayo yaliyo letwa na kampuni ya TBL.

Naye diwani wa Kata ya Tunduma, Frank Mwakajoka, aliwataka wahudumu katika Hospitali hiyo kuilina miundombinu ya maji ili idumu na kutumika kwa kizazi hadi kizazi katika mji huo na kuwa haitakuwa vizuri kama mradi huo utaharibiwa mapema.

Related Posts