SIKU chache baada ya Jeshi la polisi kupitia IGP Ernest Mangu kupiga marufuku vikundi vya ulinzi vilivyoanzishwa na vyama vya siasa hapa nchini, Kiongozi wa mafunzo wa kikundi cha Red Briged (CHADEMA) wilaya ya Momba (TUNDUMA), mkoani Mbeya, Methius Mwafongo, @ RASTA, amekamatwa akiwa na vifaa vya Jeshi la ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Mbali na vifaa vya kijeshi ambavyo alikamatwa navyo zikiwemo sare za Jeshi hilo, pia alikutwa na mapanga, Manati na mawe yake.
Wakati tunaenda mitamboni, kuna taarifa kuwa, Katibu wa Itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mbeya, Bashiru Madodi, amekutana na waandishi wa habari mchana wa leo na kuzungumzia tukio hilo na kuitaka serikali kufanya uchunguzi wa kina zaidi.

Alipotafutwa kwa njia ya simu, Madodi amekiri kukutana na waandishi wa habari na kwamba amethibitisha taarifa za kuwepo kwa tukio hilo ambalo linahusisha mafunzo ya vijana 600 kila wilaya ya mkoa wa Mbeya kwa nia ovu.
“Chadema mara kadhaa wamenukuliwa kuwa nchi hii haitakalika, haya bila shaka ndiyo mafunzo wanayoyaandaa hivyo naitaka serikali kupitia vyom,bo vyake vya ulinzi na usalama vifanye uchunguzi wa kina kila mkoa na kuwachukulia hatua stahiki za kisheria kwa yeyote anayetaka kuharibu nchi” alisema Madodi.
Aidha alieleza kuwa kuna taarifa chama chake kimezipata pia kuwa, mafunzo hayo ya vijana wa Chadema, yanalenga kuwatisha wapiga kura kila Jimbo ili wasiweze kujitokeza kujiandikisha na kupigia kura kura ya maoni katiba inayopendekezwa vinavyotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Baadhi ya viongozi wa Chadema ambao hawakutaka majina yao kuandikwa, wamekiri kuwepo kwa mafunzo mbalimbali na kukamatwa kiongozi huyo na kwamba viongozi wa ngazi za juu wanafanya mpango wa kuwasiliana na vyombo vya dola ili kufahamu tatizo kubwa la Mwafongo.
Mpaka sasa, kiongozi huyo wa mafunzo wa Chadema (RASTA), anahojiwa na vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mbeya.
Mtandao huu unaendelea kufauatilia na kesho utazungumza na ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kufahamu taratibu za kumfikisha mahakamani ama ataachiwa mikononi mwa Polisi