TAASISI za umma nchini zimetakiwa kulipa ankala za maji ili
kuziwezasha mamlaka za maji kutoa huduma nzuri za maji na kuhudumia watu wengi
kwa pamoja.
Akizungumza katika kilele cha maji Mkoani Mbeya Afisa wa
maji Bonde la Mto Rufiji, Idrisa Msuya ambaye alikuwa mgeni rasimi katika hafla
fupi ya kilele hicho alisema kuwa taasisi za uma zimekuwa zikisita kulipa
Ankara za maji na kujilimbikizia madeni.
Msuya alisema kuwa mamlaka za maji nchini zimekuwa
zikishindwa kutekeleza majukumuyake kwa weledi kutokana na taasisi hizo kuto
lipa Ankara za maji kwa wakati na kusababisha changamito kuto kwamuliwa katika
mamlaka ya maji.
Alisema hiyo ni changamoto inayo zikabili mamlaka nyingi za
maji hapa nchini na kuwa huenda serikali haiweki bajeti ya maji kwa taasisi
hizo ama kumekuwa na matumizi mabaya ya fedha zinazotengwa kwaajili ya maji.
Msuya pia aliwataka wananchi kutunza vyanzo vya maji ili
maji kuendelea kuwapo wakati wote hapa nchini bila kupungua hata kipindio cha
mvua zitakapo katika.
Nae Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya Maji Mkoani Mbeya
Mhandisi Simon Shauri alisema kuwa kutokana taasisi za Uma kuto lipa Ankara zao
na kuwa na madeni makubwa wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali za
kuboresha huduma za maji.
“Taasisi za umma zimekuwa na madeni makubwa ambayo mpaka
sasa mamlaka ya maji inazidai na hazija lipa kitu kinacho tupa sisi kama
mamlaka katika ufanyaji wa kazi,” Alisema Shauri.
Alisema mbali na changamoto hiyo mamlaka imekuwa ikifanya
juhudi za kuhakikisha wananchi wa jijini Mbeya wanapata maji kwa masaa kati ya
15 na 24 kwa maeneo yote ja jiji la Mbeya.
Alisema mamlaka ya maji imekuwa ikifanya ulinzi shirikishi katika
vyanzo vya maji kwa kushirikiana na jamii inayo zunguka katika vyanzo vya maji
ili kuhakikisha vyanzo vinatunzwa na kupata maji kwa kipindi chote cha mwaka.