MIRADI mingi ya halmashauri haita kamilika katika mwaka wa
fedha wa 2014 na 2015 kutokana na ufinyu wa bajeti wa jumla ya shilingi 42.3
iliyo kadiliwa kama rasimu na kupitishwa na baraza ra halmashauri hiyo.
Bajeti hiyo ambayo ilileta mvutano katika halmashauri ya
Mbeya Juzi ambapo kila diwani alimtaka mwenyekiti wa halmashauri hiyo kumpa
fedha nyingi ili kutekeleza miradi yake.
Madiwani wa halmashauri hiyo wengi walitaka miradi mingi
kutekelezwa katika kata zao lakini kutokana na ufinyu wa bajeti hiyo miradi
hiyo itakwama kwa mwaka huo.
Mwenyekiti wa halmashauri
hiyo, Andason Kabenga, alisema, kuwa madiwani wawe watulivu kwa wale ambao
hawajapewa fedha za kutekeleza miradi kwa mwaka huo wa wedha katika rasimu hiyo
na miradi yao kutekelezwa kwa mwaka wa fedha wa 2015/2016.
Alisema kuwa kuna badhi ya kata hazija tengewa fedha katika
rasimu hiyo na zilipata fedha kwa mwaka huu unaoendelea na kuisha juni.
Kwa upande wa ke Diwani wa kata ya Ilungu Hashimu Mwashang’ombe
alisema kwa mwaka wa fedha huu kata yake haijapata mradi hata mmoja, na kuwa
wengine walipata miradi mikubwa ya maji na yenye fedha nyingi.
Aliwaomba madiwani wenzake kuwa watulivu kama kwa mwaka huo
hawajapata fedha basa watabata kwa mwaka unao fuata kwani mgawanyiko unaenda
kwa kupokezana kutokana na uhaba wa bajeti.
“Niwaombe madiwani wenzangu kutokana na Bajeti yetu kuwa finyu tuwe wavumilivu na tukumbuke kuwa tunaenda kwa zamu kama ulipata mwaka jana wenzako watapata mwaka huu na wengine watapata mwaka ujao”