HALIMASHAURI ya wilaya ya Mbeya imepitisha rasimu ya bajeti
ya shilingi bilioni 42.3 ya mwaka wa 2014 na 2015 na kuweka vipaumbele katika
maendeleo na kukuza vitaga uchumi vya halimashauri.
Akisoma rasimu hiyo Mwekahazina wa halmashauri hiyo Hafithu
Mgazi alisema kuwa halimashauri ya Mbeya imependekeza rasimu ya bajeti ya
shilingi bilioni 42.3 na kuweka vipaumbele mbalimbali katika bajeti hiyo ikiwa
ni vya kimaendeleo.
Alivitaja vipaumbele vya bajeti hiyo kuwa ni pamoja na Maji,
Elimu, Barabara, kilimo na Mifugo, Afya
na ukusanyaji wa mapato ya halmashauri.
### alisema halmashauri
katika rasimu hiyo katika kipaumbele cha miundombinu ya barabara ambayo
itasaidia halmashauri hiyo kuongeza kipato na kuwasaidia wananchi huondoka na
adha ya usafiri na kutenga itaghalimu bilioni 1.2.
Alisema katika sekta ya elimu halmashari hiyo imetenga milioni
1.02 kwa ajili ya elimu msingi, shilingi milioni 221.9 imetengwa kwaajili ya
ukarabati wa miundombinu ya shule za sekondari.
Aliongeza kuwa mbali na sekta zingene halmashauri imetenga
jumla la shilingi bilioni 2.7 kwa ajili ya sekta ya afya, huku katika secta ya
maji ikitenga shilingi bilioni 4.7.
Bajeti hiyo pia imeweka vipaumbele katika uimarishaji wa
vitega uchumi vya halmashauri hiyo katika udhibiti wa ushuru wa halmahsuri
unaotegemea mazao.
Halimashau imekusanya jumla ya shilingi bilioni 9.1 sawa na
asilimia 24 ambayo ni mapato ya ndani hadi kufikia mwezi Novemba mwaka jana.
Kwa upandewake mwenyekiti wa halmashauri ya Mbeya Andason
Kabenga alisema kuwa Serikali imeambua kuziagiza halmashauri kukadilia rasimu ya mapato mapema
kabla ya kuisha mwaka wawedha ni mpango mpya wa kuweka utekelezaji madhubuti wa
mipango mbalimbali ya kila halmashauri.