Watu Watano Wafariki Dunia Mkoa wa Mbeya

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi.
WATU watano wamefariki dunia Mkoani Mbeya katika matukio matatu tofauti
likiwemo la ajali ya haice iliyosababisha vifo vya watu wanne mkoani hapa.
       
Katika tukio la kwanza gari  lenye namba za usajili  T.519 AKH aina ya Toyota Haice ikiendeshwa na dereva asiyefahamika kugongana na pikipiki yenye namba za usajili  T.535 Awc aina Ya T-Better eneo la Nanenane Jijini Mbeya. Ajali hiyo imetokea Septemba 29 majira ya  Saa 4 usiku katika eneo la Nane-Nane, Kata Ya Isyesye,  barabara Kuu ya Mbeya/Njombe .
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amewataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa mwendesha pikipiki ambaye bado jina lake halijafahamika sanjali na wengine watatu raia wa Ethiopia ambao majina yao bado hayajafahamika mara moja  ambao walikuwa wamepakizwa kwa pamoja kwenye pikipiki hiyo kwa mtindo maarufu wa Mshikaki.
Aidha Katika ajali hiyo  Edward Aloyce (42) Mkazi Wa Uyole ambaye alikuwa abiria kwenye  Haice alijeruhiwa na amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya. Kwa mujibu  wa  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ndugu Msangi amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari hiyo ya abiria pamoja na pikipiki hiyo.
Amesema  dereva wa hiace alikimbia mara baada ya kusababisha ajali hiyo ambapo jitihada za kumsaka zikiendelea kufanyika na jeshi hilo miili ya marehemu imehifadhiwa  Hospitali Ya Rufaa Mbeya.
Katika tukio jingine mtu mmoja  Mkazi wa Masoko Wilaya ya Rungwe  Ndugu Tukupyelesya Enock Mwakifuna (54) amefariki dunia mara baada ya gari walilokuwa wakisafiria  T.913AMB aina Ya Toyota Hillux ikiendeshwa na dereva asiyefahamika  kuacha njia na kupinduka  huko katika kijiji cha  Masoko, Wilaya Ya Rungwe, Mkoa Wa Mbeya bararabara ya Tukuyu/Lwangwa.
      Aidha Katika ajali hiyo abiria Watatu wanawake  wawili na Na mwanaume mmoja walijeruhiwa na wamelazw katika hospital ya  Hospitali ya Wilaya Rungwe huku chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi  dereva .
     Kufuatia matukio hayo Kamanda wa Polisi Mkoa Wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi Wa Polisi Ahmed Msangi ametoa o wiito  Kwa madereva kuwa  Makini wanapotumia vyombo vya moto ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza Kuepukika. 
CHANZO; Jamiimojablog.