SERIKALI imehahidi kutengeneza miundoiminu ya mbalimbali
ikiwemo ya barabara katika chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (Must)
ili miundombinu hiyo iendane na hadhi ya Chuo.
Hayo yamebainishw ana Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na
Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa katika maafari ya Kwanza ya Chuo hicho Mkoani
Mbeya.
Prof. Makame alisema kuwa serikali itaboresha miundoimbinu ya
barabara katika maeneo ya chuo hucho kikiwa ni pamoja na barabara iendayo
chuoni hapo ambayo haijakarabatiwa.
Alisema kuwa ili chuo hicho kiendane na hadhi yake na kuwa na
heshima serikali ianatakiwa kukarabati barabara kutoka marabarakuu ya Tanzania
Zambia hadi Chuoni hapo.
Alisema ni aibu kwa
serikali kuwa na barabara mbovu inayoenda katika chuo kinacho toa wataalam
mbalimbali hapa nchini.
Alisema chuo hicho kinatoa wataalam wanao tengeneza
miundombinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na wakandarasi wa majengo pamoja na
barabara.
“Haipendezi kwa chuo kikubwa kama hiki cha sayansi kuto kuwa na barabara nzuri wakati ndicho kinacho zalisha wataalamu wa miundombinu,” Alisema Prof. Mbarawa.
Katika maafari hayo ya kwanza ya chuo hucho Kikuu cha sayansi
Prof. Mbarawa alimteua Joseph Msambichaka Kuwa Kaimu mkuu wa chuo hicho.