UN yaomba msaada wa Dola bilioni 13

Umoja wa Mataifa umetoa ombi la kutolewa kiasi cha Dola bilioni 13 kwa ajili ya shughuli za misaada kwa mwaka ujao wa 2014. 
Katika mkutano uliofanyika Geneva, Uswisi, Mratibu wa masuala ya kibinaadamu na dharura wa Umoja wa Mataifa, Valerie Amos, amesema kuwa nusu ya kiasi hicho cha fedha kinahitajika kwa ajili ya Syria na mataifa jirani. 
Kwa ujumla msaada wa mwaka mzima utawasaidia watu milioni 52 katika mataifa 17.