Umoja wa Ulaya umekubali kutuma wanajeshi 500 katika Jamhuri ya Afrika ya Kati katika juhudi za kusaidia kurejesha amani.
Mgogoro ulianza katika Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya wanamgambo wa kiislamu kuchukua hatamu za uongozi wa nchi.
Ujumbe wa Umoja wa Ulaya utaungana na wanajeshi 1,600 wa Ufaransa na wengine wapatao 4000 kutoka mataifa ya kiafrika ambao tayari wamewasili nchini humo.
Mkuu wa Sera wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton amesema wanajeshi wao watafanya kazi katika mji mkuu Bangui kwa muda wa hadi miezi sita, wakisaidia kulinda usalama wa watu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.