Vatican yahojiwa kuhusu ukiukaji wa kingono dhidi ya watoto

Maafisa kutoka makao makuu ya Vatican wamehojiwa hadharani kwa mara ya kwanza, kuhusiana na vitendo vya unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto, vilivyofanywa na mapadri wa kanisa Katoliki
Katika mahojiano hayo, Umoja wa Mataifa umewauliza maafisa hao maswali kadhaa, ikiwemo kwa nini taarifa muhimu hazikutolewa, na nini walikuwa wanafanya kuzuwia ukiukaji katika siku zajazo.
Vatican ni mwanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watoto, ambao unatekelezwa kisheria, na unayalinda makundi ya kijamii yaliyo hatarini zaidi.
Mjumbe wa Vatican katika Umoja wa Mataifa Askofu Silvano Tomas amesema vitendo vya udhalilishaji watoto kingono haviwezi kukubalika, na hiyo ndiyo sera ya Vatican ya muda mrefu. 
Makao makuu ya Vatican yamesisitiza jana kuwa yamedhamiria kukomesha vitendo vya unyanyasaji wa kingono miongoni mwa viongozi wake wa kidini.