Iran yatimiza matakwa kuhusu mpango wa nyuklia

Shirika la Kimataifa la Kudhibiti Nishati ya Nyuklia, IAEA limesema kuwa Iran imesimamisha shughuli za kurutubisha madini ya urani. Waangalizi wa shirika hilo walisema jana kuwa nchi hiyo imepiga hatua ya kwanza katika mpango wa kupunguza mpango wake wa nishati ya nyuklia. 
Hatua hiyo imefungua mlango kwa mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Umoja wa Ulaya na Marekani kuidhinisha ahueni katika vikwazo vilivyowekwa na nchi hizuo dhidi ya Iran.