Showing posts with label Iran. Show all posts
Showing posts with label Iran. Show all posts
Ndege iliyo anguka Iran yaua watu 40

Ndege iliyo anguka Iran yaua watu 40



Ndege ilioanguka nchini Iran

Ndege moja iliokuwa na abiria 40 imeanguka mjini Tehran nchini Iran.
Runinga ya taifa la Iran imesema kuwa abiria wote wamefariki .
Ndege hiyo ya kampuni ya Taban Air imeripotiwa kuanguka katika makaazi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Mehrabad Maghribi mwa mji wa Tehran.
Ndege hiyo inayojulikana kama Iran 141 ilitengezwa nchini Iran kupitia teknologia ya Ukraine.
Uchunguzi umeanzishwa kuhusu ni nini kilichosababisha ajali hiyo.
Iran imekabiliwa na ajali kama hizo katika siku za hivi karibuni kutokana na ndege zake zilizozeeka mbali na marekebisho mabaya inazozifanyia.
 Iran yatimiza matakwa kuhusu mpango wa nyuklia

Iran yatimiza matakwa kuhusu mpango wa nyuklia

Shirika la Kimataifa la Kudhibiti Nishati ya Nyuklia, IAEA limesema kuwa Iran imesimamisha shughuli za kurutubisha madini ya urani. Waangalizi wa shirika hilo walisema jana kuwa nchi hiyo imepiga hatua ya kwanza katika mpango wa kupunguza mpango wake wa nishati ya nyuklia. 
Hatua hiyo imefungua mlango kwa mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Umoja wa Ulaya na Marekani kuidhinisha ahueni katika vikwazo vilivyowekwa na nchi hizuo dhidi ya Iran.
 Iran kuhudhuria mkutano wa Syria-UN

Iran kuhudhuria mkutano wa Syria-UN



Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Iran

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban ki-moon ameikaribisha Iran katika ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa amani kuhusu Syria utakaofanyika wiki hii, hatua iliyousababisha upinzani mkuu kutishia kuususia mkutano huo.
Muungano wa kitaifa wa upinzani Syria, unapinga kuhusika kwa Iran, lakini Ban ki Moon anasema anaamini kwamba Iran inapaswa kuwa sehemu ya suluhu ya mzozo huo.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa alituma mwaliko huo kwa serikali ya Iran, baada ya kushauriana kwa zaidi ya siku mbili na waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif, ambaye amekubali kuhudhuria mkutano huo.
Kujihusisha kwa Iran kunamaanisha nchi zote ambazo zimetajwa kuhusika kwenye vita hivyo vya syria,zitahudhuria kongamano hilo la kimataifa litakalofanyika mjini Montreuz nchini Uswizi siku ya Jumatano.
Tangazo hilo la Iran limetoa matumaini katika juhudi za kusitisha vita hivyo vilivyodumu kwa zaidi ya miaka mitatu, baada ya baraza la upinzani la Syria SNC kuamua kuhudhuria.
Mazungumzo kati ya serikali ya rais Bashar al assad na upinzani yanatarajiwa kuanza mjini Geneva siku ya Ijumaa.

Fedha za Iran na Saudia Arabia

Iran ni mfadhili mkubwa wa fedha na vifaa vya kijeshi kwa serikali ya rais Bashar al Assad.
Bwana Ban pia ametuma mwaliko sawa na huo kwa serikali ya Saudi Arabia, ambayo hufadhili upinzani nchini Syria.
Akiongea na waandishi wa habari katibu huyo mkuu wa umoja wa mataifa amesema, wameafikiana na waziri wa mambo ya nje wa Iran, kuwa dhamira kuu ya mazungumzo hayo, ni kukubaliana kuhusu serikali ya mpito itakayokuwa na mamlaka.
Serikali ya Marekani na mataifa mengine ya Magharibi yalikuwa yamepinga Iran kuhudhuria mkutano huo ikiwa itakataa kuidhinisha azimio lililosaini na mataifa yenye ushawishi makubwa duniani tarehe thelathini juni mwaka wa 2012.
Azimio hilo liliidhinisha kubuniwa kwa serikali ya mpito nchini Syria.
Lakini serikali ya Iran imesema kuwa itawakilishwa kwenye mkutano huo mradi hamna vikwazo vyovyote.

ULIMWENGUNE TENA HII IRAN IMETOKEA

HUYU BINADAMU MWANAUME HAJAOGA MIAKA 60 MUWONE ANAVYOFANANAZZZ LIVE!!


Iranian man hasn't had a bath in 60 years
PHOTOSAn Iranian man has broken the world record for the number of years spent without bathing. He spent the last 60 years without a bath. The Iranian News Agency (IRNA) recently published pictures of the 80 year old man.




Mzee huyu Amoo Hadji anaishi katika kijiji cha  Dezhgah Wilaya ya Dehram district jimbo la Fars nchini Iran. Anaishi kwa kula mizoga ya wanyama na kitu kikubwa anachopenda ni kutumia kiko kuvuta kinyesi kikavu cha wanyama. Pia anapendelea kushinda kwenye shimo lilichimbwa kama kaburi kwenye mwamba wa mawe na pia huvaa helmet asikiapo baridi na kuwasha sigara nyingi kwa wakati mmoja.(Picha zote na Mohammad Babaei, Islamic Republic News Agency)


























In its report, the agency noted that the man, Amoo Hadji, lives in the village of Dezhgah in the Dehram district of Fars province in Iran.
The man eats dead animals, and his most prized possession is his pipe, which is 3 inches in diameter, in which he smokes animal dung. Amoo Hadji lives in a stone shack built for him by his neighbors and he rests in a hole in the ground resembling a grave.
The news agency also noted that when he feels cold, he wears a helmet and lights up several cigarettes at a time.
Source: Al-Sharq. Photos by Mohammad Babaei, Islamic Republic News Agency
NA BLOGGU YA WANANCHI

Kategori

Kategori