ELIMU inatakiwa kutolewa kwa wananchi kuhusiana na mipaka na
maeneo ambayo yametengwa na serikali ili kuondoa migogoro vijijini na matatizo yanayo
tokana na mipaka ya ardhi.
Washiriki semina kwa maafisa Ardhi nyanda za juu kusini |
Hayo yalibainishwa na
Kaimu Mkurugezi wa Mipango ya Vijiji wizara ya ardhi, Nyumba na maendeleo ya
Makazi, Simiton Ijukaine, wakati akizungumza waandishi wa habari muda mfupi
baada ya kumaliza kutoa elimu kwa maafisa ardhi wa Nyanda za juu kusini alisema
kuwa elibu ndogo ndio chanzo cha kuwapo kwa migogoro ya ardhi vijijini.
Ijukaine alisema kuwa wananchi wamekuwa wakiingia katika
migogoro baina yao wenyewe ama serikari kutokana na kuto jia mipaka ya eneo
analomiliki.
Alisema kuwa wananchi wamekuwa wakijenga na kufanya shughuli
za kibinadamu katika maeneo ambayo
serikali imeyapima na kuweka kwaajili ya kufanyashughuli zingine au kuwekwa
kwaajili ya kuhifadhi.
“Kuto kuwepo kwa elimu wananchi wamekuwa wakiingia matatizoni kutokana na wananchi kuto jua maeneo ambayo ni tengevu na kupimwa na serikali na wengune kujenga maeneo mabayo tayali yalikuwa yanamilikiwa,” alisema Ijukaine.
Hivyo kufuatia migogoro hiyo Ijukaine alisema kuwa serikali
imeamua kuanza kutoa elimu kwa maafisa ardhi ili nao kutoa elimu kwa wananchi
nchini kote na kusaidia kuwapo kuwapo kwa upungufu ama kuondoa kabisa migogoro
ya ardhi.
Alisema kuna maeneo ambayo yalipimw ahapo awali na serikali
na kuweka alama na wananchi kuto jua kama eneo hilo liliwekwa alama.
“Kuna maeneo mengine nimetembelea yalisha pimwa na serikali na kuwekwa alama miaka mingi lakini wanakijiji hawajui au alama ambazo zilipimwa eneo lile zimeondolewa unakuta wanakijiji wamejenga ama wanaendelea na shughuli zingine kama kilimo bila kujua kama eneo lile lilipimwa inapo kuja serikali kusema eneo lilipimwa ngogoro ndio unaanzia hapo,” aliongeza Ijukaine.
Aidha Ijukaime aliitaka
serikali na halimahauri za vijiji na wilaya kuwafahamisha wananchi maeneo
ambayo yalipimwa awali na halimashauri hizo na kutembelea kila wakati ili
kuwasaidia wananchi kuto ingia katika maeneo hayo na kuepusha migogoro na
wananchi isiyo na sababu.