Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi Mbeya, Bashiru Madodi |
UWANJA wa Sokoine kutochezewa mechi mbili za mwanzo
ukisubiliwa kuwa imara kwa kuchezewa mpira kufuatia matengenezo yaliyofanyika.
Akizizungumzia sababu za kutochezea mpira kwa msimu huo
ambapo umeomwa kutochezewa kwa muda wa wiki mbili, Katibu wa CCM Mkoa wa Mbeya,
Bashiru Madodi alisema Chama cha Mpira Mkoa wa Mbeya (Mrefa) kimeomba kutochezwa mechi Mbili.
Madodi alisema kuwa uwanja huo uliofanyiwa marekebisho
katika sehemu kuu mbili sehemu ya kuchezea na Magoli umekamilika na kuwa
unaweza kuchezewa mpira.
Kutokana na kuto kuwa vizuri uwanja huo Mrefa wameomba kwa
Chama cha mpira Taifa TFF kuhahilisha kuchewa mechi Mbeli zilizo takiwa
kuchezwa uwanjani hapo.
Alisema Mrefa
wameomba kuahilisha mechi hizo mblili kufuatia kuto komaa vizuri kwa nyasi
zilizo pandwa na kuwa wananchi wasiwe na wasiwasi kufuatia kuto cheza kwa mechi
hizo mbli za awali.
Kufuatia ukarabati huo ukiwa ni wa awamu ya kwanza kufanyika
Madodi alisema kuwa kutakuwa na awamu ya pili ambayo itahusisha ukarabati wa
vyoo kiwanjani hapo.
Madodi alisema kuwa ukarabati uliofanywa uwanjani hapo
umekuwa ni mkubwa kuwahi kutokea na TFFwamesema kuwa sasa uwanja wa Sokoine
unaonekana kuwa ni miongoni mwa viwanja bora vya mpira hapa nchini.