WAATAALAM kutoka katika halimashauri mbalimbali za Nyanga za
juu kusini wamezitaka taasisi za kibenki kuzitabua hati za kimika kutoa
mikopoko.
Wakichangia kwa nyakati tofauti wakati wa majumuisho ya semina
ya siku tatu kwa wataalam hao uliofanyika jijini Mbeya, walisema kuwa taasisi
za kifedha zinatakiwa kutabua hati za kimila.
Walisema kuwa hati za kimala hazitakuwa na maana kamataasisi
za kifedha hazita zitambua kwani hati hizo zipo kisheria.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugezi wa Mipango ya Vijiji wizara
ya ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi, Simiton Ijukaine, (Pichani) alisema kuwa
kutokana na kuwapo kwa hati hizo zinazotambulika kisheria ilipashw ana taasisi
za kifedha zifanye hivyo hivyo.
Alisema kuwa hata taasisi za kifedha zikitambua uwepo wa hati
hizo za kimila zitasaidia wananchi kuwa katika hali nzuri za kupata mikopo na
kuboresha maisha yao.
Alisema mbali na utabuaji wa hati hizo aliwageukia wananchi
hao kuweka vizuri maeneo yao kwa kuweka vitu vyenye thamani vitaweza kusaidia
taasisi za kifedha kutoa mkopo wa thamani ya juu.
Ijukaine aliongeza kuwa taasisi za kifedha zitatoa mkopo
kufuatia kuwapo kwa vitu vyenye thamani kama mazao ya kudumu, nyumba na miti.
Mmoja wa maafisa wa ardhi alisema kuwa taasisi za kifedha
zinaangalia thamani ya kitu kilichopo katika ardhi iliyopewa hati.
Nao baadhi ya maafisa
walisema kuwa jina la hati hiyo nalo linachangia kuwapo kwa kuto kuiamini
hatihiyi inayo fahanika kama hati ya kimila.