MTU anayedaiwa kuwa na upungufu wa akili amemjeruhi kwa
panga Bibi kizee (80) sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo kichwani na
kusababisha kifo chake wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Makandana
wilayani Rungwe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi alisema kuwa
marehemu alivamiwa na Hosea Mwaiswelo anayedaiwa kuwa na upungufu wa akili
mkazi wa maeno hayo.
Alisema kuwa Marehemu alijerukiwa kwa kukatwa na panga
kichwani na katima mkononi kabla ya kupelekwa hospitalini.
Akisimulia tukio hilo Msangi alisema kuwa marehemu akiwa
nanakula ndani kwakwe na mjukuu wake Esta Kitwika (9) mwanafuzi wa darasa la
nne walivamiwa ndani na mtuhumiwa huyo.
Alisema mwanafunzi huyo wa shule ya msingi Syukula nae
alijeruhiwa na mtuhumiwa huyo na alipatiw amatibabu kisha kuruhusiwa.
Alisema kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na jehi la polisi na
atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Msangi aliongeza kuwa chanzo cha tukio hilo kinachunguza na
kuitaja jamii ya wakazi wa Mbeya kuwa makini wanapokuw ana watu wenye ugonjwa
wa akili na kuwapeleka hospitalini ili kuepukana na madhara kama hayo.