BAADHI ya wakazi wa jiji la Mbeya wamekuwa na maoni tofautu kufuatia ukarabati wa barabara ya Kutoka Kituo kikuu cha Mabasi mpaka maeneo ya Meta kufuatia barabara hiyo kuanza kuwekwa vilaka muda mfupi baada ya kufumuliwa na kujengwa upya.
Barabara hiyo ambayo ilifumuliwa na kuanza kujengwa upya muda wa miezi miwili iliyopita imeanza kuwekwa vilaka vya zege baada ya kuonekana inaitrafu katika baadhi ya maeneo.
Mmoja wa wakazi wa jiji la Mbeya ambaye ni dereva wa daradara Hasan Mwakalebule, alisema kuwa barabara hiyo haijamaliza hata miezi miwili imeanza kuwekwa vilaka.
Alisema barabara hiyo kwa maeneo mengi imeanza kuvimba na kutoa mipasuko ambayo inasababisha barabara kuonekana kama ya zamani.
Nae dereva Tax na mkazi wa jiji la Mbeya ambaye amekuwa akiitumia barabara hiyo mara kwa mara, Bakari Ramadhani, alisema kuwa mkandarasi anatakiwa wawajibishwa kutikana na ubovu wa barabara hiyo ambayo imeanza kuharibika kabla haijamaliza hata miezi miwili.
Kwa upande wake mkurugezi wa halmashauri ya jiji la Mbeya, Musa Zungizo alisema kuwa barabara hiyo ameiona matatizo hayo na ametoa taarifa kwa mkandarasi ili afuatilie tatizo nini linalo sababisha kuumuka kwa barabara.
Alisema kuwa ameiona barabara hiyo ikiwa ina umuka kwa baadhi ya maeneo na kuwa barabara hiyo bado haijakabidhiwa.
Alisema barabara hiyo kunamaeneo ambayo yanaonekana kuwa yanamaji mendi ndombani inafanya hiyo kutokana na mvua maji yameingia chini.
Alisema baada ya mkandalasi kupitia na kujua kitaalamu zaidi ndio atakuwa na jibu la tatizo hilo kitaalam zaidi.
“Mimi huwa nazunguka kila leo katika barabara zote za jiji na kuangalia barabara hizo nimeona katika barabara ya Stendi kuu mpaka maeneo ya Meya kuta matatizo nimemtaarifu mkandarasi wa jiji ili afuatilie na ataniambia kitaalamu,” alisema Zungizo.
Aliongeza kuwa mkandarasi aliye pewa barabara hiyo bado hajalipwa kwani barabara huwa inakabidhiwa baada ya kukaa kwa muda wa miezi 12 ndipo inakabidhiwa kwa serikali.