KAMANDA Ahmed Msangi ametakiwa kuendeleza utamadundi wa
aliyekuwa jkamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya wa kushirikiana kwa ukaribu na
waandishi wa habari mkoa wa Mbeya.
Hayo yamebainishwa Juzi na Chama cha waandishi wa habari
wakati wa hafla fupi ya kumuaga aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya
Diwani Athumani.
Akizoma risala fupi
ya waandishi wa habari Katibu wa chama cha waandishi wa habari, Emmanuel
Lengwa alisema kuwa Kamanda Msangi afuate nyayo za Athumani katika ufanyaji
kazi na waandishi wa habari.
Alisema, Athumani alikuwa akifanyakazi kwa ukaribu na
waandishi wa habari ambapo alianzisha mfumo mpya wa kutuma matukio yanayo tokea
mkoani Mbeya kwa njia ya Barua pepe kila siku wa waandishi wa habari Mkoani
humo.
Alisema kwa matumizi hayo mazuri ya mtandao na teknoloji
waandishi wa habari kwa kipindi alichokuwepo Athumani waandishi walikuwa
hawalazimiki kufika katika ofisi za Polisi kufuata matukio.
“Athumani ametumia ipasavyo mfumo huu wa kidijijali kwani amekuwa akiwarahisishia waandishi wa habari kupata matukio kwa njia ya mtandao na kuwarahisishia ufanyaji wa kazi,” alisema Lengwa.
Lengwa alimuomba, Msangi kufuata utaratibu huo ambao
waandishi wa habari Mbeya walianza kuuzoea kupata matukio bila kupata usumbufu.
Alisema kwa mambo aliyoyafanya ndiwani Athumani hata
makamanda wa Polisi katika Mikoa mingine Tanzania wafanye hivyo ili kuepusha
usumbufu kwa waandishi wa habari na kwa ofisi ya Polisi kwa kuongeza mda wa
kufanya kazi na jamii muda ambao walikuwa wakiutumia kuzungumza na waandishi wa
habari.
“Kwa kutumia mtandao waandishi wa habari wamekuwa wakitumia mda mwingi kufanya mambo mengine kwa muda waliokuwa wakiutumia kwenda Polisi na jeshi la polisi limepunguza gharama za kutumia kila siku karatasi za kuchapishia matukio,” aliongeza Lengwa.