Wanafunzi
watano wa shule ya sekondari Mustafa Sabodo iliyopo nje kidogo ya mji
wa Mtwara wamefariki Dunia na wengine 47 kujeruhiwa baada ya kugongwa na
gari wakati wakikimbia mchakamchaka mapema leo asubuhi.
Taarifa inasema kuwa gari hilo lenye namba za usajili T174 AED aina
ya Mercides Benz lilikuwa likiendeshwa na Dereva Baraka Mgwegwe ambapo
likiwa kwenye mwendo kasi liliacha njia na kuwagonga wanafunzi hao ambao
walikuwa kandokando ya barabara wakikimbia mchakamchaka kurejea
shuleni.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara Zelothe Steven na Mganga Mkuu wa
hospital hiyo wamethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na amewataja
wanafunzi waliopoteza maisha kwa ajali hiyo ni pamoja na Khairati
Mohamed Said, Mwanahamisi Mohamed,Nasma Salum Mpunja, Hilda Matias Nguli
na Farida Ally ambao wote wanasoma kidato cha kwanza katika shule hiyo.
Mpaka sasa hali za majeruhi 21 waliolazwa hospitalini hapo
zinaendelea vizuri ukiondoa mmoja ambaye amehamishiwa katika hospitali
ya mission Nyangao mkoani Lindi kwa matibabu Zaidi huku dereva
aliyesababisha ajali hiyo akishikiliwa na polisi kusubiri sheria kufuata
mkondo wake.
Dereva Baraka Mgwegwe ameongea na millardayo.com na
kusema>>’Nimetoka nyumbani kwangu sa 10 na nusu alfajiri naelekea
kumpeleka Mgonjwa Lindi Hospital nilikuwa na ndugu zangu wawili na
mgonjwa kwenye gari,tulipofika maeneo ya Pacha ya kwenda Mchuchu mbele
yangu kulikua na lori imesimama na nyuma ya lori ndio kunasadikiwa kuwa
kulikuwa na hao wanafunzi’
‘mimi nilikuwa nimejiandaa kupishana na hiyo lori na wanafunzi na
wanafunzi nao wanaingia barabarani sehemu ambayo mimi nilikuwa najiandaa
kupita mimi sikumuona mwanafunzi hata mmoja kilichotokea pale nikutokea
kwa hiyo ajali ya kuwagonga hao wanafunzi baada ya kuwagonga nikaenda
kusimama kama mita 20 kutoka eneo la tukio nikatafuta usafiri wa piki
piki nikaja kituoni hapa’.
Hizi ni picha za baadhi ya wanafunzi waliolazwa hospital ya mkoa wa Mtwara kufuatia ajali hiyo.
Hii ni taarifa ya Jeshi la polisi Mkoa wa Mtwara.