BARAZA la Madiwani wa halmashauri ya Mbeya, lipitisha pendekezo la kuajiriwa kwa mtaalam mshauri kwa ajili ya kusimamia mapato ya ndani, baadhi ya madiwani wameonesha wasiwasi juu ya ajira hiyo.
Wakipisha bajeti ya mwaka wa fedha 2014/15 katika kikao cha baraza la madiwani jana Jijini hapa, madiwani hao walisema kuanzishwa kwa ajira hiyo mpya ni mzigo kwa halmashuri.
Halmashauri hiyo imepitisha makadirio na makisio ya bajeti ya kiasi cha shilingi bilioni 45.3, ambazo ni fedha za ruzuku toka serikali kuu, pamoja na makusanyo ya ndani katika halmashauri hiyo.
Akichangia hoja ya kuajiliwa kwa mtaalam mshauri, diwani wa kata ya Tembela, Leonard Mwasile, alisema kitendo cha kuanzisha ajira mpya imedhihirishwa wazi kuwa watendaji waliopo hawana uwezo.
“Mwenyekiti sisi tuna timu ya ufuatiliaji katika suala la ukusanyaji mapato, sasa inakuaje tutafute mtu mwingine wa kufanya kazi hiyo….na kama hali ni hiyo basi naomba tuelezwe kama halmashauri imeajili watu wasio na utaalam” alihoji Mwasile.
Aliongeza kuwa hali hiyo inaiongeza mzigo wa matumizi ndan I ya halmashauri jambo ambalo limekuwa changamoto ya muda mrefu, ambapo matumizi yamekuwa makubwa kuliko ukusanyaji.
Kwa upande wake, diwanmi wa kata ya Tembela,Festo Mwalyego, alisema badala halmashauri kutoa ajila mpya ni bora ikateua mtendaji mmoja toka idara ya fedha ambaye atafanya kazi hiyo.
Kufuatia hofu hiyo, ofisi ya Ofisa tawala (Ras) mkoa wa Mbeyas,ililazimika kuingilia kati na kutolea ufafanuzi juu ya hoja hiyo.
Akifafanua zaidi, mwakilishi wa katibu tawara wa mkoa wa Mbeya , Ezekia Kilemte, alisema serikali iliamua kutoa pemndekezo hilo baada ya kushauriwa na ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti wa hesabu za serikali (CAG) kufuatia kubainika kwa changamoto .
Alisema katika ukaguzi wake, ofisi ya CAG imekuwa ikibaini kuwepo upungufu mkubwa wa ukadiliaji na makisio ya vyanzo vya mapato unaofanywa na watendaji ndani ya halmashauri.
Kutokana na hali hiyo iliishauri serikali kutoa pendekezo la kuajiriwa kwa mtaalam mshauri ambaye atasaidia kuzishauri halmashauri katika mapendekezo yao mbalimbali ya bajeti zao ili kuepuka kutofikiwa kwa malengo na kuibua migogoro dhidi yao na wanasiasa.