ASKARI wawili Mkoani Mbeya wamepandishwa kizimbani katika
mahakama ya hakimu mkazi ya Mbeya wakiwa na watu watatu kwa mashitaka ya kunyanyanya
kwa kutumia silaha.
Washitakiwa hao watano wamepandishwa kizimbani mbele ya
Hakimu Mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Mbeya, Michael Mteite kwa kosa moja la
kutumia siraha kuwateka na kuwapola vitu watu watatu wakiwemo watu wawili raia
wa India kinyume cha sheria kifungu cha 287 sura ya 16 kama ilivyofanyiwa
marekebisho waka 2002.
Mwendesha mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa aliwataja washitakiwa
hao kuwa ni Askari Polisi PC James Musa mwenye namba F8302 wa Wilaya ya Mbeya ambaye
ni mshitakiwa namba moja.
Aliwataja wengine kuwa ni Elinanzi Mshana(22) Mkazi wa Iyela
Jijini Mbeya, Askari Magereza mwenye namba B 500 Sajenti Juma Mussa(37) wa
Gereza la Ruanda Mbeya,Mbaruku Hamis(29) Mkazi wa Iyela na Amri Kihenya(38)
Mkazi wa Iyela.
Akisoma mashtaka yao Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama
hiyo, Mteite, Mulisa alisema washitakiwa hao walitenda kosa hilo Januari 3,
Mwaka huu majira ya saa 11 jioni katika eneo la Kawetere barabara ya Mbeya-
Chunya.
Alisema washitakiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo kwa
kulizuia gari aina ya Pick Up lililokuwa likiendeshwa na Ezekia Matatira (34)
Mkazi wa Iyunga Jijini Mbeya ambaye alikuwa na mtu aliyekuwa akifahamika kwa
jina la Sreedhar Pasupelet(38) mwenye asili ya Raia wa India wakitumia magari
madogo mawili ambayo ni GX 100 Toyota Cresta T 782 BEU na Gari lingine ambalo
lilikuwa na namba za Chesesi GX 6011832 AINA ya Grand Mark II.
Aliongeza kuwa mbinu iliyotumika ni washitakiwa hao kuegesha
gari moja katikati ya barabara huku wakidai gari inapancha na kuhitaji msaada.
Baada ya wahanga kusimama waliwaporwa vitu vyao wakiwa na
kwakutishiwa mapanga amapo wahanga waliporwa pesa shilingi Milioni 3.5, Mabegi
matatu yenye nguo mbali mbali, Kompyuta mpakato, simu aina ya Sumsung yenye
thamani ya Shilingi Laki mbili pamoja na simu ya Dereva aina ya Tecno ambayo
aliitambua Mahakani na kutumika kama kielelezo.
Hata hivyo watuhumiwa wote kwa pamoja walikana kuhusika na
matukio hayo ambapo upande wa Mashtaka ulileta Shahidi mmoja ambaye ni Dereva
wa Pick up Ezekia Matatira.
Akiieleza Mahakama tukio hilodereva huyo kama shahidi namba moja
aliwatambua washtakiwa wote watano na kuwa siku hiyo ya tukio aliagizwa na Bosi
wake kwamba awapeleke wageni Chunya na ndipo alipotekwa katika eneo hilo huku
watekaji kabla ya kumshusha kwenye gari yake walimfunga pingu mkono wa kuume na
kumtishia kwa panga.
Aidha kutokana na kesi hiyo Hakimu Mteite aliahirisha kesi
hiyo hadi Januari 15, mwaka huu ambapo upande wa Mashtaka utaleta mashahidi
wengine huku watuhumiwa wakirudishwa Rumande baada kutokana na kosa lao kuto
kuwa na dhamana kisheria.