KESI YA ASKALI YASIKILIZWA LEO



 

KESI inayowakabili watu watano wakewemo askali wawili kwa makosa wa ujambazi, inayoendeshwa katika mahakama ya wilaya ya Mbeya jana imeendelea ka kusikiliza shahidi wa pili.
 
Kesi hiyo imesikilizwa mahakamani hapo ikiwa ni siku ya pili baada ya kuahilishwa marambili kufuatia kuuguwa kwa mshitakiwa namba wa Pili, Elinanzi Mshana(22)  ambaye alipigwa risasi ya paja  lake la mguu wa kulia baada ya siku ya kwanza kusikilizwa shagihidi wa kwanza katika kesi hiyo.

Mbele ya hakimu Mfawidhi Michael Mteite shahidi wa pili ambaye ni Mkuu wa upelelezi wa wilaya ya Mbeya, OC-CID Mtatilo, akitoa ushahidi wake katika mahakama ya wilaya ya Mbeya alisema yeye siku ya tukio alisimamia ugaguzi wa gari walizokuwemo washitakiwa.

Alisema kuwa yeye alisimamia ukaguzi katika hali hizo mbili ambazo zilidaiwa kuwa zilitumiwa na washitakiwa wakati wa tukio hilo na kuvitaja vitu ambavyo vilikutwa katika gari hizo mbili.

Mtatilo aliiambia mahakama kuwa katika gari ya kwanza walikuta kuna mabegi ya nguo Kopyuta ndogo mblili (Laptop) pamoja na simu na gali hiyo.

Alisema katika gari ya pili ambayo ilitumika katika tukio hilo ambayo inadaiwa kutumika na mshitakiwa wa pili, Mshana  ilikutwa na blanket mbili za kisasa ambazo zimedaiwa kuwa zilipolwa wakati wa tukio hilo.

Gari zote mbili zimewekwa mahakamani kama kielelezo cha mahakamani hapo na vitu vingine vyote vilivyo kutwa wakati wa ukaguzi wa magari yaliyokutwa na washitakiwa.

Wakili wa upande wa utetezi wa washitakia katika kesi hiyo, ladslaus Lwekaza alitoa kipingamizi wakati Mtatilo alipotaka hati ya ukaguzi kuingizwa katika moja ya vielelezo vya kesihiyo kutokana na karatasi zilizotumika ukaguzi hazikuwa zilezinazotakiwa kutumika ambazo zinakuwa zimechapishwa.

Mtatilo alisema kuwa sababu ya kutumika karatasi hizo ni kutokana na siku ya tukio mshitakiwa wa pili alikuwa akivuja damu na kutakiwa ukaguzi kufanyika haraka na kufanya ukaguzi chini ya sheriaya ukaguzi namba 42 kifungu cha kwanza (b) kifungu kidogo cha (ii) ambacho kinazungumzia ugaguzi wa dharula na kuomwa kitumike kama kielelezo.   

Kesi hiyo inawakabili askali wawili wa Jeshi mmoja akiwa ni askali wa jeshi la Polisi,James Musa na askali wa jeshi la Magereza Juma Mussa na watu wengine watatu Elinanzi Mshana, Mbaruku Hamis, Amri Kihenya wakazi wa jijini Mbeya