MKUU WA WILAYA YA MBARALI AWASHAURI WANANCHI

MKUU wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya, Gurahamuhussen Kifu amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuchagua viongozi wanao wawakilisha vizuri.
Hayo yamebainishwa katika Mkutano na wafanya biashara wa mji mdogo wa Rujewa, uliowahusisha wataalamu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kitengo cha elimu kwa mlipakodi.
Alisema kuwa wananchi ili wawakilishwe vizuri katika maamuzi na kutungiwa sheria zilizo na maslahi kwa maendeleo yao.
Alisema kuwa wananchi wamekuwa wakikumbana na sheria ndogondogo zinazowabana mbavu katika mazingira yao ya kila siku ya ufanyaji kazi.
Alisema sheria hizo ndogondogo zimekuwa zikisababisha migongano baina ya wananchi na watendaji wa halmashauri wakati wa utendaji na utekelezaji wa sheria hizo.
Kifu alisema kuwa wananchi wakichagua kiongozi mbovu wanakutwa na majanga makubwa wakati watendaji wa halmashauri wakitekeleza sheria hizo zilizotungwa na viongozi walio wachagua wenyewe.
Hayo yaliibuka baada ya mamlaka ya Mjo mdogo wa Rujewa kutangaza kuwa kutakuwa na sheria ndogo itakayo wataka wananchi kuwa na vikapu vya kuwekea taka na kulipa fedha wakati wa kuchukuliwa takazizo na mtoa taka.
Kwa mfumo huo na sheria hiyo itasaidia mamlaka hiyo ya mji mdogo kuwa na usafi wa hali ya juu na kuondokana na utupaji taka hovyo.