Tulikutana na kundi kubwa la Mbega weupe karibu na Kituo cha Mandara wakati tukishuka Mlima Kilimanjaro kwa njia ya Marangu mwaka jana (2013). Lilikuwa ni kundi la mbega wapatao 15 hivi lakini wengi walikuwa wamejificha kwenye miti ya msitu unaozunguka kituo cha Mandara. Huyu mmoja ndio alikuwa amekaa eneo la wazi ambapo niliweza kunasa taswira zake. Walitupa burudani nzuri ya kelele na manjonjo yao kwenye miti.
Habari Online na Elimtaa
Habari za utalii wa ndani
Utalii wa Ndani na Elimtaa: White Colobus Monkey (mbega Weupe) wa Mlima Kilimanjaro
Subscribe to:
Post Comments (Atom)