MABWENI
waliyokuwa wakiishi wanafunzi 355 wa shule ya Wenda yameteketea kwa moto
uliozuka katika mabeni hayo katika maeneo ya Mbalizi halmashauri ya Mbeya na
kuteketeza vitu mbalimbali.
Akizungumza
na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi alisema
kuwa tukio hilo lilitokea Juzi katika Shule Wenda iliyopo maeneo ya Mbarizi
halmashauri ya Mbeya.
Alisema Mkurugezi wa Shule hiyo Fideles Daniel (54) majira ya saa 2:15 usiku aligundua moto katika mabweni ya shule hiyo.
Mabweni
yaliyo teketea katika shule hiyo yalikuwa na majina tofauti tofauti, Koffi
Annan na Marcus kwenye mabweni haya moto ulidhibitiwa kwa kuzimwa na wanafunzi
pamoja na watu wanaoishi jirani na shule hiyo kwa kushirikiana na kikosi cha zima
moto.
Alisema, kuwa mabweni ya State House na Malcom X yaliteketea kabisa kwa moto na hakuna kitu kilichookolewa katika mabweni haya.
Wakati
moto huo unaanza kuteketeza mabweni hayo wanafunzi walikuwa katika vyumba vya
madarasa wakijisomea muda wa usiku.
Alisema
kuwa chanzo cha moto huo bado hakijajulikana na kuwa thamani ya vitu vilivyo
teketea inaenelea kuchunguzwa.
Msangi
alisema kuwa mabweni yaliyoteketea yalikuwa yakilaliwa na wanafunzi wanaume na
kuwa jumla ya vitanda 74 vimeteketea.
Kamanda
amewataka wamiliki wa shule na taasisi zingine kuwa na vifaa vya kuzimia moto
ilikukabiliana na matukio ya aina hiyo yanapo tokea.