Polisi watoa ufafanuzi kuhusi mabox yaliyo kamatwa





JESHI  la polisi mkoani Njombe limeamua kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi  waliokua amelizingila gari ya serikali ambayo haijafahamika ya idaragani, lililokuwa linadhaniwa kuwa na kura zilizopigwa tayari na baada ya kukabuliwa kumebainika kukuta fulana za chama cha mapinduzi zenye picha za mgombe wa Urais.


kizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Wilbroad Mutafungwa alisema kuwa Jeshi hilo lililazimika kutumia Mabomu baada ya wananchi kulizingira gali lililozaniwa kuwa ni gari lililobeba kura zilizopigwa.

“Asubuhi ya leo tulilikamata gari lililokuwa linazaniwa linadhaniwa kuwa linakura zilizo pigwa sio sahihi mule mulikuwa na Tiseti za chama cha mapinduzi (CCM), na lilikuw ana tisheti za chama hicho,” alisema Mutafungwa.

Mutafungwa alisema kuwa jeshi la polisi liliwatawanya wananchi hao na na kuondoka na baadhi ya viongozi wa Chadema na wale wa chama cha Mapinduzi (CCM) kuelekea katika ofisi za polisi kisha kuanza kufanya ukaguzi wa mabox hayo na kubaini kuwa zilikuwa ni fulana za chama cha CCM.

Alisema kuwa jeshi hilo lilifanya upekuzi wa mabox hayo yaliyo kuwa yakitokea Jijiji Dar es Salaam kupitia kampuni ya Don Don ya usafirishaji baada ya kugunduliwa na wananchi  kuwa ni gari ambayo inabox za kura.

Alisema kuwa walifanya ugaguzi ka pamoja na kuzikuta box 10 zenye tishet zaidi ya 200 kwa kila box na kuwa hawakukuta karatazi ya kura hata moja katika Box hizo.

Aidha kwa kupande wake mwenyekiti wa CCM wilaya ya Njombe Mjini Abuu Mtamike alisema kuwa walizipata taarifa za kuwa kunagari ina karatasi za kura zilizo pigwa na kuwa baada yak u;likamata gari hilo waliamua kuwapigia Polisi na kulikamata gari hiyo kisha kuikagua na kukuta tisheti za ccm zenye picha ya mgombea Uraisi John Magufuli.

Alisema kuwa walipata taarifa hizo na kufuatilia taarifa hizo kisha kulikamata gari hilo kwa ushirikiano na jeshi la polisi.

Kwa upande wa chama cha CCM mweyekiti wake wa mkoaHosea Mpagike, ambaye alikuwepo katika ukaguzi wa gari hiyo alisema kuwa gari alipigiwa simu kuupokea mzigo huo wa Tisheti  kutoka makao makuu ya chama na kuwa baada ya kufika katika mkoa wa Njombe alipigiwa simu kuwa mzigo huo umekamatwa.

Alisema kuwa mzigo huo ulikuwa ukuwa uende katika jimbo la Wanging’ombe ambako zilitakiwa kupfanyiwa kampeni za kufunga na kuvaa wanachama wake jana katika kufunga kampeni zake.