Njombe Hawaja waelewa Twaweza na Utafiti wao

BAADHI ya wakazi mkoani njombe Wameukandia utafiti uliofanywa na taasisi ya Twaweza na kusema kuwa utafisti huo umelenga kuwachanganya na kuwa hawaukubari.

Wakizungumza na Nipashe Mkoani Njombe baadi ya wakazi wa mkoani humo wamesema kuwa utafiti huo umeibeba CCM na kuwa hawaamini njia iliyo tumika kufanya utafiti huo.

Mmoja wa wakazi hao Joel Mhagama mkazi wa ChaugiNgi Mkoani Njombe alisema kuwa twaweza walifanya utafiki kwa watu wanao ikubari CCM na wamenaya utafiti kwa ubaguzi kwa kuwa wangefanya utafiti huo katika maeneo ambayo kunamchanganyiko wa watu.

"Utafiti huo wangepita Mfano katika maeneo ya Stend, wangepata majibu sahihi kuliko walivyo sema wamepitia katika maduka huenda kuna watu wamejibu kwa uoga wa kupoteza biashara zao," Alisema Joel.


Alisema kuwa utafiti huo umerkuja kuwavuruga watanzania na kusema kuwa utafiti huo ni wa uongo kutonana na hali ya kisiasa ilivyo katika harakati za uchaguzi CCM wanavyo jaza watu na Ukawa wanavyo jaza watu.


Alisema kuwa kwa watu walio wachaguwa kuwahiji hawawezi kuwawakilisha watanzania wote na kuwa watu kwa sasa mpaka vijijini wameamka hawapo tena CCM wapo Chadema na Ukawa.

Aidha wengine ambao hawakutaka kutajwa majina yao wameungana na kauli ya Mgombea Uraisi kupitia Chadema na anayeungwa mkoni na Umoja wa katiba ya Wananchi Ukawa Edward Lowassa kuwa matokeo kamili ni baada ya uchaguzi utafiti ni wauongo na hawauamini.